FA imewaomba msamaha Harry Kane na Smalling

Chama cha soka England FA JANA kimetangaza rasmi kufikia maamuzi ya kuwaomba msamaha wachezaji Chris Smalling wa Man United na mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane kufuatia tweet yao waliyoipost kupitia account yao ya twitter kutafsirika tofauti.
FA wameomba radhi kufuatia jumbe wao waliopost baada ya mchezo wa nusu fainali ya FA kati ya Tottenham dhidi ya Man United uliyomalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-1, ambapo ujumbe huo unatafsirika kama ulimkosea heshima Harry Kane na Smalling.
Tweet yao ilikuwa inasomeka “Nini kipo mfukoni mwako” halafu inaonekana Smalling anajibu ni “Harry Kane” kitu ambacho kilitengenezwa kwa lengo la utani tu  wakimaanisha kuwa Smalling amefanikiwa kumdhiniti Harry Kanekatika mchezo dhidi yao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment