Maalim Seif Apigwa Marufuku Mwanza

CHAMA cha Wananchi (CUF) mkoani Mwanza kimempiga marufuku Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kutofanya mikutano na vikao vya kisiasa katika wilaya za Nyamagana na Ilemela zilizoko jijini hapa.

Hatua hiyo ya kumpiga marufuku Maalim Seif aliyesimamishwa uongozi na Baraza Kuu la Uongozi la CUF Taifa, imetolewa katika tamko la pamoja la viongozi katika wilaya za Ilemela za Nyamagana mkoani Mwanza.

Viongozi hao waliongozwa na Mwenyeviti wa CUF wa Wilaya ya Nyamagana, Salum Mkumbukwa aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa, Martha Haule na Zainabu Ally.

Walidai kuwa wamesikia kuwa Maalim Seif anawasili jijini Mwanza kwa siri kupitia mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la kuhudhuria kongamano moja la chama cha siasa linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni katika wilaya za Nyamagana na Ilemela akiwa na lengo la kukutana na wanachama wa CUF, jambo ambalo uongozi halina tija kwa wakati huu wakati akiwa amesimamishwa uongozi.

Viongozi hao walisema wamemwandikia barua Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela kupinga ujio wake
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment