Mbunge CHADEMA Ahoji Bungeni sababu za ripoti za CAG kutokuwa na taarifa za Tanroads Shirika la Ndege (ATCL)

Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), amehoji bungeni kuhusu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutokuwa na taarifa za Shirika la Ndege (ATCL) na Wakala wa Barabara (Tanroads).

Akichangia bungeni jana mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha, mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, alisema hakutarajia kuona ripoti ya CAG ya mwaka 2016/17 ikikosa taarifa za taasisi hizo muhimu katika kipindi hiki ambacho zinatengewa fedha nyingi.

Alisema taarifa za fedha za taasisi hizo zilipaswa kuwamo kwenye ripoti ya CAG ili wahoji kama wanavyofanya sasa kuhusu kutoonekana kwa matumizi ya Sh. trilioni 1.51.

Silinde ambaye alihoji ni sababu za ripoti za CAG kutokuwa na taarifa za Tanroads ili wabunge waangalie barabara za Tanzania kama zinaendana na thamani ya fedha inayotolewa.

“Sisi kama wabunge tunatakiwa kuhoji kwanini katika ripoti ya CAG huwa hakuna Tanroads, tunatakiwa kuhoji; je, barabara inayojengwa inalingana na 'value for money' (thamani ya fedha)?” alisema Silinde.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment