Bunduki Ya Kivita Yaokotwa Vichakani

Bunduki ya kivita aina ya AK 47, ikiwa na risasi nne ndani imeokotwa ndani ya vichaka katika Kijiji cha Naan, Wilaya ya Ngorongoro mjini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi amethibitisha kuokotwa kwa silaha hiyo na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka mmiliki wake.

“Mbali na bunduki hiyo, pia tumekamata pikipiki saba zinazodhaniwa kuwa ni mali ya wizi na watuhumiwa saba kupitia msako tuliofanya hivi karibuni,” amesema.

Kamanda Ng’anzi amezitaja mali zilizokamatwa kuwa ni televisheni sita, camera tatu, lensi mbili za camera, fedha taslimu Sh 915,000 na vitu vingine vya ndani na vifaa ofisini.

Pamoja na mambo mengine, Kamanda Ng’anzi amewaomba wakazi wa Arusha waliowahi kuibiwa kufika kituoni hapo ili kukagua kama wanaweza kutambua mali zao
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment