Lukuvi Apiga Marufuku Kampuni Za Kupima Ardhi Kudai Wananchi Gharama za Upimaji

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amepiga marufuku makampuni yanayopima ardhi yasiwadai wananchi gharama za upimaji wa ardhi.

Amesema kila makampuni hayo yatakapokuwa yakipima ardhi yatatakiwa kulipwa fedha za upimaji kupitia kwenye vikundi vilivyochaguliwa na wananchi.

Lukuvi ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo, alipokuwa akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2018/19.

“Aidha, wapimaji hao wanatakiwa kutoa taarifa katika uongozi wa wilaya husika kuhusu uwepo wao katika maeneo wanayopima ardhi,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Lukuvi aliwahimiza wananchi kuwa na kawaida ya kulipa kodi ya ardhi kila mwaka kwa kuwa ni wajibu wao kisheria.

“Kwa upande wa wananchi wanaokabiliwa na migogoro ya ardhi, nawaomba wafike kwa maofisa wa wizara yangu ili migogoro yao iweze kutatuliwa haraka iwezekanavyo,” amesema Lukuvi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment