Makonda: Nimelelewa jeshini ndio maana mimi ni jasiri

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amebainisha kuwa baba yake ni moja kati askari kutoka Tanzania ambao wamepigana vita nyingi kwa ajili ya kutetea taifa ikiwemo vita ya Kagera mwaka 1978.

Makonda amesema hayo wakati alipokuwa anatoa salamu kwa Rais Magufuli katika sherehe za ufunguzi wa kituo cha uwekezaji cha SUMA JKT Mgulani Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa alizaliwa na kulelewa katika kambi za jeshi

“Nikunong’oneze mheshimiwa Rais, mimi nimezaliwa kambini na baba yangu ni miongoni mwa askari waliopigana vita nyingi ikiwemo vita ya Uganda na mpaka ulemavu wake wa mguu ni kutokana na kazi ya kuipigania Tanzania,” amesema Makonda

Aidha, Makonda ameongeza kuwa kutokana na kulelewa katika kambi za jeshi imemsaidia kupata ujasiri wa kuongoza mkoa wa Dar es salaam wenye changamoto nyingi na kuweza kufanya kuwa Jiji la raha Tanzania.

Katika tukio hilo, Rais Dkt Magufuli alizindua kituo cha uwekezaji cha SUMA-JKT ambacho ndani yake kuna kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha Ufundi Stadi na Ukumbi wa Mikutano
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment