Maofisa watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini (Tanzania Investment Center (TIC) wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia jana Mei 22, 2018 maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.
Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana amesema ajali hiyo imehusisha gari ya serikali STK 5923 aina ya Toyota land cruiser lililongana na Scania T620 AQV ambaye dereva wake alihama kwenye njia yake na kusababisha ajali hiyo.
Waliopata majeraha ni wawili Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus
0 comments :
Post a Comment