Mbunge Ahoji Serikali ‘kung’ang’ania’ Ng’ombe Jimboni Kwake

Mbunge wa Itilima, Njalu Silanga (CCM), amehoji ng’ombe 339 katika Jimbo lake kuendelea kushikiliwa na Serikali wakati mahakama iliamuru waachiwe huru.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Silanga amesema wafugaji wameteseka hususani wa kando kando ya hifadhi huku akitaka miundombinu katika minada iboreshwe ili iwasaidie wafugaji kusafirisha mifugo.

“Kwenye Wilaya yangu ya Itilima ng’ombe 339 wa wafugaji wanashikiliwa na serikali waKati mahakama iliamuru  waachiwe, mambo haya yapo kisheria lakini tunadhulumiwa baadhi ya vyombo vinazuia ng’ombe zetu Waziri tusaidie kwanini jambo hili linaendelea.

“Ukiachilia mbali suala la ng’ombe, katika maeneo yetu hatuna miundombinu mizuri nia yetu ni ya dhati lakini lazima msaidie wafugaji lakini pia nikupongeze Waziri kwa mipango yako ya kuhakikisha Kiwanda cha Shinyanga kinafanya kazi,” amesema Silanga
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment