Mzee wa Upako Ampigia Simu Q-Chief ,Ni Baada ya Kusikia Anaacha Muziki.

Baada ya kuweka wazi dhamira yake ya kuacha muziki, msanii Q Chief amesema amepigiwa simu na watu wengi mmoja wapo ni Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’

Muimbaji huyo amesema kuwa Mzee wa Mpako alionyesha kuguswa na hatua hiyo aliyoamua kuichukua.

“Nimepokea simu kutoka kwa mtu kama Anthony Lusekelo, usiku saa tisa, unaweza kuona ni jinsi gani mchungaji anaweza kuguswa na kusema mwanangu nimetaka kama kulia hivi, nimepigiwa simu na maostadhi wakubwa sana Tanzania hii,” Q Chief ameiambia Clouds TV.

Ameongeza kuwa amefikia maamuzi hayo na hana kinyongo chochote na mtu ila kwa sasa ameona mapenzi makubwa sana kutoka kwa watu kwenda kwa Q Cheif
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment