Leo May 18, 2018 Kamati Maalum ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imebainisha kuwa ilipata wasi wasi kuhusu madeni yanayolikabili Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), lakini wamejiridhisha liko vizuri kutokana na miradi inayoendeshwa.
Akizungumzima wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Nape Nnauye amesema kuwa awali walipata wasi wasi kuahusu shirika hilo kutokana na maneno yaliyokuwa yakisemwa.
Nape ambaye ni mbunge wa Mtama, amesema awali Kamati ilikuwa na wasiwasi kwa sababu walisikia shirika linadaiwa madeni kuzidi thamani ya shirika lenyewe.
“Ilitupa wasiwasi ndio maana tukaomba ripoti, lakini pia tukaomba tuje kujionea wenyewe ambapo tumejiridhisha kwamba shirika liko vizuri na thamani ni kubwa,”- Nape Nnauye
Nape amesema kamati inalipongeza shirika hilo, lakini pia inaiomba serikali kukamilisha Sera ya nyumba ili kurahisisha baadhi ya vitu.
0 comments :
Post a Comment