Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, amesema matukio ya uhalifu yanayotokea nchini yanawafanya baadhi ya wawekezaji wasije kuwekeza nchini.
Amesema pamoja na kwamba Tanzania inaweza kuwa na jitihada za kuwashawishi wawekezaji kutoka nje waje kuwekeza nchini mkakati huo unaweza usifanikiwe kwa kuwa wawekezaji wanapenda kuwekeza katika nchi zenye usalama kuliko katika nchi zenye vurugu na mauaji.
Sugu amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Mei 23, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyowasikishwa na Waziri wa Wizara hiyo Augustine Mahiga.
Sugu alimtaka rais aanze kusafiri kwenda nje kwa sababu safari za nje zina faida kama ilivyowahi kutokea enzi za Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliyekuwa akisafiri mara kwa mara.
“Lakini pamoja na hayo, serikali haiwatendei haki Watanzania wanaoacha kazi nje na kuja kufanya kazi nchini kwa sababu inataka iwalipe mishahara midogo kama ilivyotokea kwa bosi mmoja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) (aliyemtaja kwa jina la Kairuki),” amesema Sugu
0 comments :
Post a Comment