Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wanawake wa mkoani humo kutokubali kuolewa na wanaume ambao wanaviwanja mabondeni.
RC Makonda ametoa kauli hiyo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua uharibifu wa nyumba zilizovunjika eneo la Kingugi kwa Mnyani Kata ya Kilungule baada ya wakazi kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
Aidha RC Makonda amewaagiza Wenyeviti wote wa mitaa kuainisha nyumba zilizojengwa kwenye maeneo hatarishi ambapo amewataka kutoruhisu watu kujenga maeneo ya mabondeni.
Katika kutafuta mwarobaini wa tatizo la wananchi waishio mabondeni RC Makonda ameandaa mkutano wa wananchi wote waishio maeneo ya mabondeni kwaajili suluhisho la kudumu.
0 comments :
Post a Comment