Kauli ya Serikali Kuhusu Milioni 50 Kwa Kila Kijiji

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema ahadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji itaanza kutekelezwa mara baada ya mfumo wa kuanza kuzitoa utakapokamilika.

Dk Mpango ametoa kauli hiyo jana jioni bungeni wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Karagwe (CCM), Innocent Bashungwa aliyoitoa wakati Bunge likiwa limekaa kama kamati kupitia vifungu kwa vifungu vya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/19.

Bashungwa alisema, “Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020, tulitoa ahadi ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji.” “Bajeti ya mwaka 2016/17 ilitengwa Sh60 bilioni na mwaka 2017/18 ilitenga Sh60 bilioni lakini mpaka sasa hazijaenda, nataka kujua kwa nini hazijaenda?”

Akijibu hoja hiyo, Dk Mpango alisema, “ni kweli jambo hili ni ahadi ya chama na ninaomba nikumbushe kwamba ni ahadi ya chama kwa kipindi cha miaka mitano
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment