Na Hezbon Mahaulane
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amempongeza waziri mkuu mpya wa Italia Giuseppe Conte. Hata hivyo ameonekana kupuuza wito ya Italia kutaka Umoja wa Ulaya kuisamehe madeni yake
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amempongeza waziri mkuu mpya wa Italia Giuseppe Conte. Hata hivyo ameonekana kupuuza wito ya Italia kutaka Umoja wa Ulaya kuisamehe madeni yake
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alifanya mazungumzo na waziri mkuu mpya wa Italia Giuseppe Conte Jumamosi na kumkaribisha mjini Berlin kwa mazungumzo zaidi kuhusu mustakabali wa uhusiano wa nchi zao.
Kwenye tarifa, ofisi ya kansela imesema Merkel alimpongeza Conte kwa kuwa waziri mkuu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Merkel na Conte walizungumza kwa njia ya simu, walitilia msisitizo umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa pande zote mbili.
Conte ambaye ni profesa wa shera asiyejulikana sana, amekuwa kimya tangu alipoapishwa . Lakini alitangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa, kando na Merkel pia alizungumza na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Jumamosi.
Amesema atakutana na viongozi hao katika mkutano wa kilele wa G7 utakaofanyika Canada, ambapo pia atazungumzia masilahi ya raia wa Italia
0 comments :
Post a Comment