Moto Wateketeza Maduka Lamadi Mkoani Simiyu

Na Hezbon Mahaulane
 Moto ambao unadaiwa chanzo chake ni mfanyabiashara mmoja kusahau kuzima pasi ya umme na kushika moto, umesababisha hasara kubwa baada ya kusambaa na kuteketeza vitu mbalimbali kwenye maduka sita katika mji wa lamadi uliopo wilaya ya busega, mkoani simiyu.

Moto huo ambao ulizuka majira ya saa mbili kasorobo usiku wa kuamkia juni 03, chanzo chake kinadaiwa ni mfanyabiashara mmoja kusahau kuzima pasi ya umme ndani ya duka na kushika moto, na hivyo kusambaa na kuunguza vitu mbalimbali, ambapo maduka sita yameteketea.

John balale ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hili, anasema jeshi la polisi  kituo cha lamadi, zima moto na wananchi  walishirikiana kuuzima moto huo lakini changamoto ikawa ni vifaa duni.

Mkuu wa mkoa wa simiyu anthony mtaka, amefika katika eneo la tukio na kujionea athari za moto huo, na kuwataka  wahanga kuwa na subira  ,wakati tathimini ya mali iliyoteketea ikifanyika, huku akiwapongeza juhudi za wananchi wa lamadi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuuzima.

Kamanda wa  jeshi la zimamoto na ukoaji mkoa wa simiyu gerevas fungamali, akizungumzia tukio hilo, anasema elimu ya zima moto na uokozi itaendelea kutolewa kwa wananchi ili kujikinga na majanga, huku diwani wa kata ya lamadi laurent bija, akiwataka wananchi kujiandaa kujikinga na majanga yanapotokea.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment