TANZIA: Mapacha walioungana Maria na Consolata wamefariki Dunia

Usiku wa June 2, 2018 Mapacha wawili walioungana, Maria na Consolata wamefariki dunia ukatika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa walikokuwa wakipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya wa Iringa Richard Kasesela,  mapacha hao wamefariki wakipishana kwa takribani saa 2.

"Wamepigania sana afya zao, mida ya saa moja hivi jioni ndio nilipokea taarifa za kifo chao na kwa sababu nilikuwa mazingira ya hospitali basi nilisogea kuwaona – na ni kweli hatunao,” amesema Kasesela.

Pacha wa kwanza alifariki majira ya saa 1 usiku, huku mwenzake akifariki saa 3 usiku.

Mapacha hao wamekuwa na historia ya matatizo ya moyo. Tangu Disemba 2017 pacha hao walianza kuumwa na kulazwa hospitali ya mkoa ya Iringa.

Baadaye walihamishiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walipolazwa kwa takribani miezi miwili kwa ajili ya matibabu mpaka waliporuhusiwa kurejea tena Iringa mnamo Mei 17.

Maria na Consolata walizaliwa wilayani Makete mkoani Njombe mwaka 1996.

Walihitimu darasa la saba katika shule ya msingi Ikonda, kisha wakajiunga na shule ya Maria Consolata iliyopo Kilolo mkoani Iringa ambapo walihitimu kidato cha nne.

Baada ya hapo, walijiunga na shule ya Sekondari ya Udzungwa wilani Kilolo walipohitimu kidato cha sita, ikifuatiwa na Chuo Kikuu cha Katoliki cha Ruaha (Rucu) walipokuwa wakisomea fani ya ualimu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment