Mwekezaji katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji anapenda kutoa taarifa kuwa ameanzisha tuzo ambazo zitakuwa zikitolewa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki wa klabu ya Simba ambazo amezipa jina la Mo Simba Awards. Kwa mara ya kwanza tuzo hizi zitatolewa siku ya Jumatatu, tarehe 11 Juni, 2018 katika hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro iliyopo Jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zitakuwa na vipengele 16, ambavyo ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka, Beki Bora wa Mwaka, Kiungo Bora wa Mwaka, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, Shabiki Bora wa Mwaka na Tuzo ya Heshima. Tuzo zingine ni Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka, Tuzo ya Benchi la Ufundi, Kiongozi Bora wa Mwaka, Tuzo ya Wasimamizi wa Mchakato wa Mabadiliko, Mhamasishaji Bora wa Mwaka katika Mitandao ya Kijamii, Mhamasishaji Bora wa Mwaka na Tawi Bora la Mwaka. Washindi wa tuzo hizo watatokana na kura ambazo zitapigwa na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii na tovuti ya mosimbaawards.co.tz na kamati maalumu ya tuzo ambayo itahusisha wadau mbalimbali wa mchezo wa mpira wa miguu nchini. Akizungumza kuhusu tuzo hizo, Dewji amesema ameanzisha tuzo hizo kwa lengo la kutambua mchango wa wachezaji, viongozi na mashabiki ambao juhudi zao zimeiwezesha Simba SC kupata mafanikio iliyonayo sasa. Dewji amesema tuzo hizo ni sehemu ya mikakati yake ya kuifanya klabu ya Simba kuwa timu kubwa barani Afrika, ambayo itakuwa na uwezo wa kifedha ambao utaiwezesha kuwa na wachezaji na benchi la ufundi bora ambalo litaiwezesha kushinda mataji makubwa. “Simba ni timu kubwa inastahili kuwa na tuzo zake ambazo zitakuwa zinatolewa kwa kutambua mchango wa wenzetu ambao umetuwezesha kupata mafanikio haya ikiwepo kushinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Ni jambo ambalo litawatia moyo kuendelea kujituma lakini hata kwa ambao watakosa itawatia hamasa na hivyo kuongeza juhudi,” amesema Dewji. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo itakuwa mbashara kupitia Azam. Imetolewa na; Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Mo Simba 2018
Neema Kwa Wachezaji, Mashabiki na Viongozi wa Simba SC....Mo Dewji Kaanzisha Tuzo Kwa Ajili Yao, Taarifa Iko Hapa
Mwekezaji katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji anapenda kutoa taarifa kuwa ameanzisha tuzo ambazo zitakuwa zikitolewa kwa wachezaji, vi...
Read More
CUF 'Yawashambulia' Wabunge Wake Wanaomtetea Maalim Seif
Chama cha Wananchi (CUF), kimewatuhumu wabunge wa chama hicho kwa kile ilichodai wamekuwa wakitetea na kulinda hadhi ya Katibu Mkuu wa c...
Read More
Mbunge Stephen Ngonyani ( Profesa Majimarefu ) afiwa na mkewe
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu 'Profesa Majimarefu’ leo Jumatano Juni 6, 2018 amefiwa na mkewe, Mariam aliyeku...
Read More
Mwanajeshi wa Tanzania auawa huko Jamhuri ya Kati Afrika
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kati Afrika wanaotokea nchini Tanzania, ameuawa na waasi huku wengine 18 wak...
Read More
Waziri Ndalichako : “Maria na Consolata ni Mashujaa wa Taifa”
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa Mapacha walioungana Ma...
Read More
Serikali Yalitaka Baraza la Maaskofu KKKT Kuufuta Waraka wa Pasaka
Serikali ya Tanzania imelitaka Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Tanzania kufuta waraka lililoutoa ...
Read More
Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako alivyomwaga machozi msiba Maria na Consolata
Miili ya mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, imeagwa kati...
Read More
Bungeni: Serikali Kujenga Kituo Kikubwa cha Kupoozea Umeme Jimbo la Kibamba
Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) inatarajia kujenga kituo kikubwa cha kupoozea umeme katika Jimbo la Kibamba baada y...
Read More
Bungeni: Serikali Yatangaza Neema ya Ajira kwa Wataalamu Sekta Ya Umwagiliaji
Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inatarajia kuwaajiri wataalamu wa kutosha katika fani ya umwagiliaji....
Read More
PICHA: Basi lagonga treni...7 Wafariki Dunia
Watu 7 wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma. A...
Read More
Alieua mateka afa akiwatoroka polisi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, limemuua kwa kumpiga risasi mtu anayedhaniwa kuwa kiongozi wa kundi la watekaji na wauaji wa watu wanaot...
Read More
Kauli ya Serikali Kuhusu Milioni 50 Kwa Kila Kijiji
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema ahadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji itaanza kuteke...
Read More
Maxcom Africa – Maxmalipo Wafafanua Tatizo La Tiketi Kwenye Usafiri Wa Mwendo Kasi Tarehe 3 Na 4 Juni 2018
RPC Shana: Majambazi Nane Yakamatwa Pwani
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani JESHI la polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu nane wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa tuhuma za kuhusika na ...
Read More
Waziri Mkuu Atoa Ujumbe Mzito Kwa Wabunge
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wabunge kuonyesha mshikamano na kupendana ili waendeleze jukumu la kuishauri Serikali. Kiongo...
Read More
Raia Wawili Washtakiwa kwa Kuhujumi Uchumi Mkoani Tabora.
Watu 2 wamefikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa Tabora kwa kosa la kuhujumu uchumi. Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani jana ...
Read More
Sakaya amkingia kifua Maalim Seif bungeni......Ataka TAKUKURU Wamhoji Yeye
Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) amesema Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) imhoji yeye kuhusu fedha za chama hicho kuto...
Read More
Mashine Za EFD Zatengamaa
Wafanyabiashara wametakiwa kurejea kutumia mashine za kieletroniki (EFD) kwa kuwa hitilafu iliyokuwa imetokea imetatuliwa. Kauli hiy...
Read More
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)