Chopa ya Chadema ikiwa angani tayari kupeleka viongozi kwenye mikutano ya uchaguzi. Picha na Maktaba
Kwa ufupi
- Polisi waitaka Chadema kutotumia siku ya uchaguzi kwa madai kuwa itavuruga wanapigakura.
Kalenga. Polisi katika Mkoa wa
Iringa, imepiga marufuku matumuzi ya helkopta siku ya uchaguzi mdogo wa
Kalenga, kwa madai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kupiga kampeni.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Mungi
alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama tangu
kampeni zilipoanza hadi sasa kwa vyombo vya habari.
Mungi alisema siku ya uchaguzi siyo siku ya
kampeni na kwamba polisi hawatakubali kuona vitendo vya kampeni
vikionekana miongoni mwa wakazi wa Kalenga ikiwamo helkopta kutumika
katika jimbo hilo na watu waliosafiri kutoka mikoa mbalimbali kwa
kisingizio cha kulinda kura.
“Sasa nataka niwaeleze kuwa sheria iko wazi. Siku
ya uchaguzi si siku ya kampeni. Hatutaki kuona helkopta za vyama vyote
zenye kuashiria kufanya kampeni. Kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na
wakala wa chama kinachoshiriki katika uchaguzi huo na hao ndiyo
wawakilishi wa chama hicho na walinzi halali wa uchaguzi ni
polisi”alisema Mungi na kuongeza:
“Hatutaki kuona walinzi wa chama chochote katika
Jimbo la Kalenga. Jukumu la kulinda uchaguzi, maisha na mali ya wana
Kalenga ni la polisi, hatutaki kuona watu wasiokuwa na shughuli maalumu
wanapitapita katika maeneo ya kupigia kura”alisema.
Tume wazungumzia
Wakati Mungi akitoa kauli hiyo, Tume ya Taifa ya
Uchaguzi(NEC) ilishindwa kutoa jibu la moja kwa moja kama helkopta hiyo
itatakiwa kutumika ama la, hali iliyosababisha maswali mengi kutoka kwa
waandishi wa habari.
Majibu ya Tume yalitolewa katika mkutano
ulioitishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu
Damian Lubava ambaye kabla ya yeye kutoa ufafanuzi alitaka wajumbe
wenzake kutolea majibu.
Akijibu swali la matumizi ya Chopa liloulizwa
katika mkutano huo, Jaji Mstaafu John Mkwawa alisema “Matumizi ya vyombo
vya usafiri tume haijakataza, ila mtu hapaswi kutumia kitu chochote
kinacholeta hali isiyo nzuri na kusababisha usumbufu, chopa inaweza
kusababisha kelele”alisema.
Naye Profesa Amon Chaligha alisema matumizi ya
helkopta ni sehemu ya kampeni na kuongeza kuwa kimsingi isingeruhusiwa
kutumika siku ya kampeni.
Akifafanua, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema vyombo vyote vya usafiri
vinaruhusiwa kutumika siku ya kampeni, lakini kwa namna ambavyo
vitatofautina na namna vilivyokuwa vikitumika wakati wa kampeni.
“Kama Helkopta itapangiwa utaratibu
utakaotofautiana na ule uliotumika wakati wa kampeni,…kumpelekea mtu
kuruka kutoka uwanja wa ndege na kwenda eneo husika bila ya kuathiri
kuonesha mazingira ya kupiga kampeni hapo sawa, lakini sheria inasema
siku ya uchaguzi siyo siku ya kampeni” alisema.
1
|
2
|
3
|
4
Next
0 comments :
Post a Comment