Imeandikwa na Nkupamah blog
leo jion m/kiti wa bunge maalum la katiba alijikuta katika wakati mgumu na kumradhimu kuahiri
sha kikao cha bunge mpaka kesho saa kumi jioni mara baada ya mjumbe mahusu
si na mtaalam wa sheria maarufu kuomba mwongozo wa mwenyekiti juu ya ukiukwaji mkubwa wa kanuni na taratibu zinazoongoza shughuli nzima za bunge hilo na kumtuhumu moja kwa moja Mwenyekiti huyo pasipo kumung'unya maneno kuwa kiti cha bunge hilo kinapwaya kwakushindwa kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa ,hivyo haoni sababu na hayuko tayari kuendelea kuburuzwa na kuendelea na kikao cha bunge kujadili jedwali lenye marekebisho ya sheria lililochakachuliwa kinyume na kanuni walizoridhiana ndani ya bunge.hata hivyo tundu lissu alienda mbali zaidi na kuiita nakala ya jedwali la marekebisho hayo ya sheria yaliyofanyika kinyume na taratibu na kanuni za bunge ni batili,uchafu,na takataka,wakati lissu akiendelea kutoa maelezo hayo sauti za baadhi ya wajumbezilisikika zikimbeza tundu lissu kwa maelezo yake ,huku tundu lissu naye akiwajibu muulizeni mwenyekiti anajua nachokizungumza,hata hivyo sitta alishindwa kuupangua mwongozo huo na kumpa nafasi mwanasheria mkuu kutoa maelezo hata hivyo maelezo yake hayakua na mashiko katika kujibu hoja ya tundu lissu,ndipo mjumbe mwingine Jussa alipoiunga mkono hoja ya Lissu kwa kusoma kanuni zilizokiukwa na kuhoji uhalali wa mabadiliko ya kanuni yaliyopo katika jedwali lililopo mbele yao,maelezo hayo yalimfanya m/kiti awe katika wakati mgumu na kumradhimu kuahirisha kikao hicho hadi kesho saa kumi jioni baada ya wajumbe kuanza kumzomea zomea.
0 comments :
Post a Comment