Written by Wamtambwe
TBC wahusishwa, UKAWA waja juu
Tayari mwenyekiti wa bunge maalum samwel sitta ameanza kuhujumu bunge hilokwa kuhujumu hotuba ya warioba leo hii.
Sitta amevunja kanuni kwa kulazimisha warioba aanze kuhutubia leo ili Rais Jk amjibu jumatano huku kanuni zikitaka rais azindue bunge kwanza ndipo warioba awasilishe rasimu rasmi bungeni. Sitaa ameshikilia msimamo wake huku ikiwa ni kinyume cha kanuni.
Pia kanuni zinataka mwenyekiti wa bunge kushauriana na mwenyekiti wa tume ya katiba kuhusu.muda unaotosha kuwasilisha rasimu. Sitta ameivunja kanuni hii kwa kumlazimisha warioba kuwasilisha rasimu kwa muda usiozidi saa moja tu leo jioni.
Aidha TBC wameingia dili na bunge na ccm kukatisha hotuba ya warioba kwa kisingizio cha matatizo ya ufundi. Hotuba ya warioba inaonekana kuwa mwiba kwa ccm na serikali.
Ukawa wamebaini hali hiyo na kuamua kuandika barua ya kutokuwa na imani na sitta barua ambayo inasainiwa now na wajumbe wote wa UKAWA ili kumtaka sitta aachie ngazi. Aidha wamepanga kuhakikisha hotuba ya rais kama itakuja baada ya warioba basi haitasomwa kwa namna yoyote.
Viongozi wa ukawa wanatoa msimamo huo soon kwa wanahabari hapa dodoma. Sitta anaelekea kuharibu kabisa mchakato huu sasa
Chanzo: JF
0 comments :
Post a Comment