Na Mussa Juma, Mwananchi
Kwa ufupi
Dodoma. Mjumbe wa Kamati ya
Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu amesema ktendo cha
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kubadilisha kanuni kwa kutoa muda zaidi wa
kuwasilishwa kwa rasimu ya katiba, kinamkera.
Lissu alisema kitendo kama hicho ndicho
kilichomfanya yeye na mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kutaka kujiuzulu
mara mbili kutokana na kupingana na wajumbe wenzao.
Akizungumza na gazeti hili jana mjini hapa, Lissu
alisema walitaka kujiuzulu kutokana na kuchoshwa na wajumbe kufikia
makubaliano ndani ya vikao, lakini wakitoka nje wanarudi na mabadiliko.
“Tulikuwa hatusongi mbele tunafanya uamuzi na
kufikia makubalino, lakini wenzetu baadaye wanaenda kujadiliana upya na
kuja na mapendekezo tofauti na kuturudisha nyuma,” alisema Lissu.
“Baada ya majadiliano yao, mimi na Jussa tuliomba
tujiondoe lakini walituomba tusijiuzulu kwa masharti kuwa
tunachokubaliana hawataweza kubadilisha.”
Alisema kile ambacho kimeanza kutokea sasa ni
kitendo cha Mwenyekiti Sitta kubadilisha kanuni ya 47 (a) ya Bunge hilo
juu ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupewa muda unaofaa
kuwasilisha rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba.
Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida
Mashariki (Chadema), alisema pia hata kubadilisha kanuni kwa kupokea
kwanza taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye ndipo Rais
Jakaya Kikwete azungumze ni jambo wanalolipinga.
0 comments :
Post a Comment