Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba wakipinga jambo ndani ya bunge juzi  
wakati Kamati namba tatu  na nne za kijadili vifungu vya rasimu ya 
Katiba walipokuwa wakiwasilisha ripoti zao
 Bungeni Dodoma juzi. Picha na
 Salim Shao 
            Posted Ijumaa,Aprili25 2014 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
“Kwanza matumizi ya lugha zisizo na staha, 
mwenyekiti anaruhusu wajumbe kuchangia hoja kwa kupeana mipasho bila 
kujali hoja iliyopo mezani kinyume na kanuni,”      
                
    
        
        
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba
 linaahirishwa leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila kupitisha hata 
ibara moja kati ya 240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba.
Badala yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta
 “Mzee wa Kasi na Viwango” linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu 
likiendelea kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita zenye jumla ya Ibara 19, 
zinazohusu masuala yanayojenga msingi wa aina ya Muungano 
unaopendekezwa.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu 
iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Jaji Joseph 
Warioba ilipendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu, pendekezo
 ambalo limeligawa Bunge hilo vipande viwili.
Kutokana na mgawanyiko huo, kauli zenye utata, 
kejeli, matusi, dhihaka na ubaguzi ni mambo yaliyoshika hatamu katika 
mjadala wa sura hizo mbili, huku viongozi wa Bunge; Sitta na Makamu 
wake, Samia Suluhu Hassan wakilaumiwa kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.
Mwanzoni mwa wiki hii, Mjumbe wa Bunge hilo, 
Ezekiah Oluoch alimshutumu Sitta kwamba ameshindwa kudhibiti nidhamu 
katika Bunge na kwamba ndiye chanzo cha kuondoka kwa wajumbe wapatao 200
 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
“Mwenendo wa Bunge Maalumu ulikuwa na dalili zote 
za kuonyesha kungetokea matatizo ndani yake kutokana na mipasho ambayo 
ilikuwa ikitokea kwa wajumbe pamoja na lugha ambazo siyo za staha wakati
 wa kutengeneza kanuni,” alisema Oluoch na kuongeza:
“Kwanza matumizi ya lugha zisizo na staha, 
mwenyekiti anaruhusu wajumbe kuchangia hoja kwa kupeana mipasho bila 
kujali hoja iliyopo mezani kinyume na kanuni,” alisema Olouch.
Hata hivyo, Suluhu alisema amekuwa akiendesha 
Bunge hilo kwa umakini mkubwa na kwamba kila anaposikia lugha chafu 
amekuwa akiwabana wajumbe kwa kuwaamuru kufuta kauli au kuomba radhi kwa
 matamshi. “Sipendezwi na lugha chafu, kwa hiyo mojawapo ya mambo ambayo
 huwa najitahidi kusikiliza kwa makini kila michango inapotolewa na 
wajumbe bungeni ni kubaini kama wametumia lugha zisizostahili, kisha 
kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni zetu,” alisema Suluhu.
Alikiri kwamba wapo baadhi ya wajumbe ambao 
wamekuwa wakigoma au kukataa kuomba radhi na kwamba masuala yao 
hupelekwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo ina mamlaka ya kuchukua hatua 
zaidi kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo.
Matakwa ya Kanuni
Sehemu ya Tano ya Kanuni za Bunge Maalumu inatoa mwongozo wa mambo yanayokatazwa na yale yanayopaswa kufuatwa wakati wa mjadala.
Kanuni ya 46 imeorodhesha mambo yasiyoruhusiwa 
ambayo ni pamoja na kusema uongo, kutoa taarifa zisizokuwa za kweli, 
kuzungumza jambo lolote ambalo halipo kwenye mjadala na kutumia majina 
ya marais na waasisi wa Taifa kwa dhihaka.
- Kwa nini malaria ni tishio kwa mama mjamzito?
- Changamoto lukuki zaiweka Tanzania njiapanda
- VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT)
- Faida za kabichi kwa afya
- Si kila homa, maumivu ya kichwa ni Malaria
- Umuhimu wa kula mboga mbichi
- Malaria huua mtoto kila baada ya sekunde 60 barani Afrika
- Wafugaji Mbeya waazimia kujikita zaidi katika elimu
- Tanzania na wasomi wasiokuwa na maadili, wanaofilisi nchi
- Heartbleed bug: Tishio jipya la uhalifu kwa watumiaji mitandao
- Maswali saba ya Jaji Warioba
- Tanzania Kwanza Nje wavurugana hadharani
- Siku 67 za mipasho, matusi bungeni
- Utafiti:Wananchi wanaunga mkono Rasimu
- JK yapuuze mambo madogo
- RC Arusha anusuru mikutano ya Lema
- Dar yapendekeza wilaya mbili mpya
- ‘Ukawa hawajalipwa posho wasiyostahili’
- Ripoti yaanika mauaji ya vyombo vya dola
- Jumuiya ya Kiislamu yaungana na maaskofu kumtetea Warioba
- TBC yapata gari la kisasa la matangazo


0 comments :
Post a Comment