MANENO YA MWISHO YA AISHA MADINDA ALIKIONA KIFO CHAKE

Stori: Gladness Mallya
SIKU chache kabla ya kupatwa na umauti, mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’ alifunguka maneno
ambayo yalionesha dhahiri kama alikiona kifo chake. Kwenye mazungumzo hayo aliyozungumza na mwanahabari wetu, Aisha alisema atatoa habari nzito ambazo zitaripotiwa na magazeti matatu na kudai ni ‘sapraiz’.
Mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’.
Licha ya paparazi wetu kumdodosa aseme habari hizo, alikataa na kusema itakuwa ni  sapraiz.
“Nina furaha sana kwa sababu nimerudi salama kutoka Dubai nilikokuwa nalazimishwa kufanya kazi za ndani nikakataa, ukweli watoto wangu wamefurahi sana kwa sababu nimerudi nikiwa na afya njema.
“Niko fiti nimeachana na madawa ya kulevya sasa hivi nimerudi rasmi kwenye kazi yangu ya unenguaji, nitakutafuta siku nikupe habari kubwa ambayo sijawahi kuzungumza sehemu yoyote yaani itakuwa ni nzuri na utatoa magazeti matatu,” alisema Aisha ambapo Desemba 17, mwaka huu alifariki dunia kabla ya kutimiza ahadi hiyo kwa mwandishi wetu.Aisha aliyeacha watoto wawili wa kiume na wa kike, alitarajiwa kuzikwa jana nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment