Friday, June 26, 2015
Nkupamah blog
Hellena Elinewinga, Mtaalam wa masuala ya utafiti, amekuwa kada wa 40 wa CCM kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho, kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumzia
hatua hiyo baada ya kuchukua fomu hiyo jana, Hellena alisema ameamua
kujitosa katika kinuanganyiro hicho, kwa kuwa anachukizwa na baadhi ya
aina ya viongozi wanaoshindwa kutoa huduma stahiki kwa watanzania na
kujinufaisha wenyewe.
Hellena
alikabidhiwa fomu hiyo jana, na Khatibu, saa 7:20 mchana huku
akisisitiza kwamba kama chama chake kitamteua kugombea kiti hicho,
atahakikisha viongozi wanaokwamisha mchakato wa maendeleo au kulihujumu
taifa, wanahukumiwa adhabu ya kifo kutokana na mchango mbovu walioutoa.
Mgombea
huyo anayefanya kazi na Asasi za Kiraia na Taasisi za Kilimo katika
mikoa ya Kanda ya Kaskazini; ni mkazi wa Tarafa ya Masama, Wilaya ya
Hai, mkoani Kilimanjaro.
Hellena
(40), sasa anakuwa mwanamke wa sita kujitosa kuomba ridhaa ya chama
chake. Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha- Rose Migiro;
Naibu Waziri wa zamani wa Fedha na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica
Mbega; Balozi Amina Salum Ali; Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu, Dk. Mwele Malecela na Ofisa Maendeleo ya Jamii,
Ritha Ngowi.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment