Friday, June 26, 2015
Nkupamah blog
Kada wa CCM, January Makamba amejikuta katika wakati mgumu na kumwaga machozi jukwaani alipokuwa akielezea historia ya maisha yake na jinsi walivyoishi na bibi yake mzaa mama katika kijiji cha Kyaka, wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.
Makamba
alipanda jukwaani juzi jioni kwa lengo la kuwashuruku wana CCM kwa
kumdhamini,lakini kabla ya hajaanza kufanya hivyo alianza kuelezea
maisha yake binafsi na bibi yake wakati huo wakiishi kijijini mwishoni
mwa miaka ya 70.
Wakati
Makamba akielezea maisha yake yalivyokuwa wakati akiishi na bibi yake,
alijikuta sauti ikikwama na kulengwa lengwa na machozi jambo
lililomfanya akatishe hotuba na kushuka jukwaani.
Kada
huyo ambaye alikuwa mkoani Kagera kusaka wadhamini, baada ya kushuka
jukwaani kwa kushindwa kuzungumza alikwenda kwenye kiti alipokuwa amekaa
na kukaa kwa muda kabla ya kurudi jukwaani tena kuendelea kutoa
shukrani kwa wanachama.
Hata
hivyo, baada ya kurudi jukwaani hakutaka tena kuelezea maisha yake na
bibi yake walivyokuwa wakiishi, badala yake alianza kuzungumzia
changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kijiji cha Kyaka pamoja
na mkoa mzima wa Kagera.
Kabla
ya kumwaga machozi jukwaani, Makamba aliwaambia wananchi hao kwamba
alikaa na bibi yake akiwa anamfundisha kulima, kusalimia watu wakubwa
pamoja na kuchunga mbuzi.
Aliwaambia
wananchi hao kwamba anayajua maisha ya kijijini kwa kuwa ameishi huko,
hivyo anadhamiria kupambana na ugumu wake ikiwa atapata ridhaa ya CCM
kugombea urais kisha kuwa kiongozi wa nchi.
“Nimeishi
huku na bibi yangu, najua maisha halisi ya huku na ndiyo maana nasema
nataka kuleta majawabu ya changamoto zinazowakabili nyinyi wananchi,” alisema.
Makamba
ambaye aliwasili kijijini hapo akitokea Bukoba mjini, alipata mapokezi
makubwa ya Pikipiki na magari binafsi ambayo yaliongoza msafara wake
hadi ofisi za CCM wilaya ya Misenyi na kupata wadhamini.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji hicho cha Kyaka walisikika wakiimba nyimbo za
Kihaya maalum kwa ajili ya kumkabirisha huku wakisema Makamba amerudi
nyumbani.
Baada
ya kupata wadhamini, Makamba alipita katika shule ya msingi ya Kyaka
ambayo alisoma kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu ambako alikutana na
mwalimu wake aliyemfundisha darasa la kwanza na kisha alielekea
nyumbani kwa bibi yake.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment