
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe (pichani), ambaye ni mmoja wa
wanachama wa CCM waliochukua fomu za kugombea kiti cha urais,
amesisitiza kuwa uamuzi wa kugombea nafasi hiyo aliufikia miaka mitano
iliyopita na kuwaomba wana-CCM kuwapuuza wale
wanaosema hakupanga kuomba
nafasi hiyo.
Waziri
Chikawe, ambaye amekamilisha kazi ya kusaka wadhamini katika mikoa 15 ya
Tanzania Bara na Zanzibar kama taratibu zinavyoelekeza, amesema uamuzi
wake wa kugombea nafasi hiyo aliufanya baada ya tafakari ya kina.
“Nilishasema
wiki kadhaa zilizopita nikiwa Nachingwea na leo ninarudia, nimetafakari
kwa miaka mitano kabla ya kuamua kugombea nafasi ya urais mwaka huu ...
ni uamuzi wangu. Kwa hiyo huo ni uzushi tu ambao unapaswa kupuuzwa,”
amesema Chikawe leo (Jumanne, Juni 6, 2015) kwa njia ya simu kutoka
Dodoma na kuongeza:
“Hao
wanaotunga hizo taarifa za uzushi ndiyo wametumwa,” amesema Chikawe
akiwa Dodoma kikazi baada ya kuombwa kutoa ufafanuzi wa taarifa
zinazosambwazwa katika mitandao ya kijamii.
Ufafanuzi
wa Waziri Chikawe unafuatia taarifa zinazosambazwa katika baadhi ya
mitandao ya kijamii kuwa hakupanga kugombea nafasi hiyo na kuwa
ameelekezwa kugombea nafasi hiyo na mmoja wa wagombea anayehofia jina
lake kukatwa na vikao vya juu vya CCM.
“Mimi si
mtu wa kulumbana mitandaoni na hata nafasi ninayoomba haihitaji mtu
mwenye hulka hiyo (ya kulumbana). Ninawaomba wananchi na wana-CCM
wenzangu wayapuuze maneno hayo kwa kuwa hayana hata chembe ya ukweli,”
amesema Chikawe na kuwasihi wananchi na wana-CCM kuwa na uvumilivu
wakati wakisubiri maamuzi ya vikao vya chama.
Pamoja na
kuwa Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Chikawe ni Mbunge wa Nachingwea.
Alihitimu shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha dar es Salaam mwaka
1965 na kufanya kazi serikalini kwa miaka mingi kabla ya kuingia katika
siasa za majukwaani na kushinda ubunge mwaka 2005 na kuchaguliwa tena
mwaka 201
0 comments :
Post a Comment