- Written by Nkupamah Blog
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakiwa
wamezungukwa na umati mkubwa wa watu wakati alipokwenda kuomba udhamini
kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Ilongero,
Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida, jana. Katika tukio hilo
maelfu ya wananchi walijitokeza kutaka kumdhamini katika harakati zake
za kuwania kuteuliwa na CCM kuwania urais. Nyalandu ambaye pia ni mbunge
wa jimbo hilo, lakini aliwataka radhi na kuomba kudhaminiwa na
wanachama 45 tu kama matakwa ya CCM yanavyoelekeza.
KATIBU wa CCM Wilaya ya Singida, Mwamvua Kilo, akizungumza wakati akimkaribisha Nyalandu kuzungumza na maelfu ya wananchi.
Nyalandu akizungumza na wananchi
WANANCHI
na wanachama wa CCM wakisikiliza kwa makini wakati Nyalandu
akizungumza masuala mbalimbali na kutumia fursa hiyo kuhamasisha umoja
na mshikamani ndani ya Chama.
WANANCHI
na wanachama wa CCM wakisikiliza kwa makini wakati Nyalandu
akizungumza masuala mbalimbali na kutumia fursa hiyo kuhamasisha umoja
na mshikamani ndani ya Chama.
WANACHAMA wa CCM wakiimba nyimbo wakati Nyalandu alipokuwa akiingia kwenye viwanja vya Ilongero kuomba udhamini
VIONGOZI
wa dini mkoani Singida, wakimpa Nyalandu mkono wa pongezi baada ya
kutoa hotuba iliyokonga nyoyo za wananchi wakati alipokamilisha kazi ya
kuomba udhamini. Mgombea huyo amepata wadhamini katika mikoa yote
nchini.
UMATI ukimsikiliza Nyalandu
0 comments :
Post a Comment