Monday, June 29, 2015
Nkupamah blog
MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Banda Sonoko, jana amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho ili kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao akiwa ni mgombea wa 42.
Baada
ya kuchukua fomu hiyo jana, Sonoko alisema kama chama hicho
kitampitisha kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao na kushinda,
moja ya vipaumbele vyake ni pamoja na kuzingatia misingi imara ya ilani
ya 2005 pamoja na kuondoa umaskini kwa Watanzania.
Sonoko
amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya Mwenyekiti wa Bodi ya
Hospitali ya Temeke ambapo katika kampeni zake za kusaka urais atatumia
kauli mbiu inayosema "Kutokomeza Umaskini".
Alisema
akiingia Ikulu, atawatimizia Watanzania mahitaji mbalimbali ambayo
wameyakosa muda mrefu ambapo yeye ana sifa zote za kuwa rais ndio maana
ameamua kuchukua fomu.
Aliongeza
kuwa atahakikisha nchi inaendeshwa kwa kodi za wananchi si misaada
kutoka nchi wahisani ambapo wanawake watawezeshwa katika mambo
mbalimbali na kupewa nyadhifa kwenye vyombo vya maamuzi pamoja na
vijana.
Sonoko
alisema Serikali ambayo ataiongoza itasimamia haki, kupinga vitendo vya
utoaji na upokeaji rushwa hasa Mahakamani ambapo kesi zitakuwa
zikiendeshwa kwa muda maalumu, kurudisha viwanda, kuinua kilimo na
kuboresha miundombinu.
"Nitahakikisha
kila Wilaya inakuwa na sehemu yake ya kuegesha magari, kuongeza ajira
na kuwasaidia vijana," alisema na kuongeza kuwa, hadi Julai mosi, mwaka
huu, atakuwa amekamilisha taratibu za kupata wadhamini 450 katika mikoa
15.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment