Tuesday, June 30, 2015
Mpekuzi blog
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema iwapo chama kitampitisha na kupewa ridhaa na wananchi kuwa rais, atahakikisha anaimarisha misingi ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano.
Alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akisaka wadhamini
huko Dimani, Mwera, Mjini na Wilaya ya Kaskazini B mjini Zanzibar.
Alisema Mapinduzi na Muungano ni mambo muhimu yanayohitaji kuenziwa na
akawataka wanachama wa CCM na wananchi kutorudi nyuma katika kuyaenzi.
“Muungano umeweka msingi mzuri wa kujenga udugu
kama kuna mashimo tutaendelea kuyafukia kwa malengo ya kuuimarisha
Muungano ili uwe imara zaidi,” alisema.
Alisema wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu, ni
vizuri suala la amani na mshikamano likapewa nafasi kubwa na wananchi
ili kulinda mafanikio yaliyoanza kuonekana Zanzibar katika nyanja za
uchumi na ustawi wa jamii.
Alisema baada ya kuzunguka Unguja na Pemba
ameshuhudia mwelekeo mzuri wa kisiasa wa CCM na kuahidi kuwa kama chama
kitampitisha na baadaye kupewa ridhaa na wananchi kuwa rais, atatumia
muda wake mwingi kuharakisha maendeleo ya visiwa vya Zanzibar.
“Pemba ilikuwa vigumu kuvaa sare ya CCM nimekwenda
kule nimeshuhudia mwenyewe hivi sasa wanachama wanavaa sare za chama
hatua hiyo ni mafanikio makubwa kwa uchaguzi wa mwaka huu,” alisema.
Alisema suala la amani lazima lizingatiwe na kutoa mfano wa
Taifa la Burundi jinsi wananchi wake wanavyoteseka na wengine kulazimika
kulikimbia kutokana na kukosekana kwa utulivu.
“Amani si jambo la kuchezewa, ona kule Burundi
wakati rais wake alipotangaza kuongeza kipindi cha tatu tu, Tanzania
tulipokea zaidi ya wakimbizi laki moja kule Kigoma kwa muda mchache,”
alisema.
Awali, Waziri Mkuu alizuru kaburi la Rais wa
Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume na Rais wa Awamu ya Nne wa
Zanzibar, marehemu Idriss Abdul Wakil aliyezikwa katika mji mdogo wa
Makunduchi Mkoa wa Kusini
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment