Tuesday, June 30, 2015
nkupamah blog
Mbunge wa Sengerema ambaye pia ameomba kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, William Ngeleja amewataka Watanzania kumpima kwa mambo 15 aliyofanya wakati wa uongozi wake serikalini. Alisema hayo jana wilayani Nanyumbu alipokuwa akisaka wadhamini.
Alisema wakati alipokuwa Naibu Waziri na baadaye Waziri wa
Nishati na Madini, aliweza kufanya mambo makubwa 15 ambayo amewataka
Watanzania wamweke katika tafakari zao na kumpima na kumwona anafaa.
Alitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni kufanikiwa
kudhibiti mgawo wa umeme ambao ulikuwa umekithiri ikiwa ni pamoja na
kuokoa kiasi cha Sh1.6 trilioni zilizokuwa zikitumika kununua umeme na
mafuta kutoka kampuni nyingine.
“Kama mzalendo wa nchi nimewania nafasi hii kwa
sababu ya historia ya utendaji wangu, Watanzania wote wanipime kwa mambo
15 ambayo nimeyafanya na ambayo yamekuwa ni faraja kwao na
kimaendeleo,” alidai Ngeleja na kuongeza:
“Baadhi ya mambo niliyoyabuni ni mradi wa ujenzi
wa bomba la gesi wakati nikiwa waziri, mradi wa umeme vijijini na
kubadili utaratibu wa kuagiza mafuta kwa pamoja ambao ulisaidia kuokoa
kiasi cha Sh600 bilioni kutokana na baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa
wakihujumu utaratibu.”
Alijigamba pia kudhibiti hasara iliyokuwa ikitokea Tanesco kutoka Sh43 bilioni hadi kufikia Sh42 bilioni, lakini baada ya kuondoka hasara hiyo ilirudi na kufikia Sh467 bilioni.
Alijigamba pia kudhibiti hasara iliyokuwa ikitokea Tanesco kutoka Sh43 bilioni hadi kufikia Sh42 bilioni, lakini baada ya kuondoka hasara hiyo ilirudi na kufikia Sh467 bilioni.
nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment