Tuesday, June 30, 2015
Nkupamah blog
Rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ametoa wosia kwa wanasiasa wanaowania uongozi katika uchaguzi mkuu ujao nchini, wawe makini na matamshi wanayoyatoa wakati wanapotafuta nafasi wanazotaka ili kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini.
Mkapa
alitoa wosia huo juzi, kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka 19
tangu kuanzishwa kwa Radio Maria Tanzania yaliyofanyika Kanisa Katoliki
Parokia ya Madhabahu ya Bikira Maria Kawekamo jijini Mwanza.
Alisema
kuelekea uchaguzi mkuu huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu,
wanasiasa wanatakiwa wachukue tahadhari na matamshi yao pale wanapowania
nafasi za uongozi ili kuepukana na uharibifu wa taifa la Tanzania.
“Taifa
likiwa linaelekea uchaguzi mkuu, naomba niwatahadharishe watu
waliotangaza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wawe makini katika
matamshi yao wakati wanapopitapita kwa wananchi na tusije tukayatoa
maneno yatakayosababisha uvurugaji wa amani yetu,” alisema Mkapa.
Aliwasihi
wanasiasa hao kuhakikisha wanazungumza kwa umakini ili kuepukana na
matamshi yanayoweza kuwagawa wengine na kuzalisha uvunjifu wa amani ya
nchi iliyopo sasa.
Aidha,
Mkapa katika madhimisho hayo, aliongoza harambee kwa ajili ya
kuendeshea kituo cha radio hiyo kiasi cha Sh. milioni 60 zinazohitajika.
Hata
hivyo, Mkapa alifanikisha kuchangasha zaidi ya Sh. milioni 40 kwa njia
mbalimbali na wadau wa ndani na nje ya nchi huku akizishauri nchi za
Afrika kujiwezesha kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wa Waafrika wenyewe
ikiwamo kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa.
Katika
hatua nyingine; Mkapa alizitaka nchi za Afrika kuacha kutegemea zaidi
misaada ya wahisani kutoka nchi za nje kutokana na baadhi kuanza
kutokana na kuelemewa na madeni makubwa.
Akihubiri
katika ibada ya misa takatifu iliyohudhuriwa na mamia ya waumini pamoja
na mahujaji 400 waliotoka hija katika eneo la Nyakibeho nchini Rwanda,
Askofu Mkuu wa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Thadeus Rwaichi,
alisema taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na
madiwani, kunapo changamoto nyingi zinazolikabili zinahitaji waumini
kusimama katika imani ya kweli na thabiti.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment