AFISA wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, PCCB, Conrad
Mtenga (53) maarufu kama Chillangamsafa amefariki katika ajali kwenye
barabara kuu ya Mbeya-Iringa.
Watu wawili wamejeruhjiwa kwenye ajali hiyo iliyotokea eneo la
Tanangozi, baada ya gari dogo aina ya Nissan Patrol, mali ya
AfriCarriers, kugongana uso kwa uso na Lori aina ya Scania.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
Iringa Pudenciana Protas alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira
ya saa 8:30 mchana eneo la Tanangozi barabara kuu ya Iringa- Mbeya
Kamanda Ptotas alisema kuwa gari hiyo yenye namba za usajili T.291
BNK aina ya Nisan Patrol mali ya Africafrie’s Ltd ya Jijini Dar es
salaam ilikuwa ikiendeshwa na Conrad Mtenga (53) maarufu kwa jina la
Chillangamsafa ambaye ni mfanyakazi wa PCCB na mkazi wa chunya. Alisema
kuwa gari hiyo iligongana na gari aina ya Scania yenye namba T.783 ATQ
ambayo ilikuwa ikiendeshwa na dereva Henry Lulandala ( 35) na
kusababisha kifo cha dereva huyo.
Majeruhi walitajwan kuwa ni pamoja na Baraka Zakayo na Rebeca Mtenga,
wote wamelazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa. Kaimu kamanda huyo
wa polisi alisema, uchunguzi wa awali unaonyesha derive wa gari dogo
alihama kutoka upande wake na kumfuata mwenye gari kubwa na hivyo
kugongana uso kwa uso.
Mabaki ya gari dogo aina ya Nissan Patrol, baada ya ajali hiyo -K-Vis Blog
0 comments :
Post a Comment