Aunt Ezekiel Awatibua Waislam

Friday, July 17, 2015

  Nkupamahmedia blog

Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ambaye jina lake la Kiislam baada ya kubadili dini ni Rahma, hivi karibuni alifanya maulidi ya kumtoa mwanaye Cookie lakini katika hali ya kushangaza alifanya mambo ambayo yaliwatibua Waislam.
 
Aunt alifanya tukio hilo hivi karibuni nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar kisha kuwaalika ndugu, jamaa na marafiki ambapo mbali na kuombewa dua na maustadhi, pia aliwafuturisha Waislam waliokuwa kwenye mfungo.
 
Licha ya kitendo hicho kilichodaiwa kuteketeza milioni kadhaa za fedha kupongezwa na wengi, katika hali ya kushangaza kuna mambo ambayo ilibainika yalikwenda kinyume na taratibu za dini ya Kiislam.
 
Kwanza
Aunt baada ya kutokea kwenye hadhara akiwa na mwanaye, alikuwa kavalia shela lilioacha wazi sehemu ya juu ya kifua na kimtandio ambacho baadaye kiliondoka na kumuacha kichwa wazi, kitu ambacho ni kinyume na Uislam.
 
Pili
Katika tukio hilo kulikuwa na ratiba ya kukata keki ambapo ulipofika muda wa yeye kumlisha mwanaume aliyezaa naye (Moze Iyobo), alimpa kwa staili ya ‘njiwa’,  jambo ambalo halikutarajiwa kufanyika katika mazingira yale.
 
Tatu
Mjadala mwingine ulihusu Aunt  kugandana na Moze Iyobo kama mume na mke wakati mtoto huyo wamempata nje ya ndoa.
Baada ya kuona na kusikia malalamiko ya baadhi ya wageni waalikwa kuhusu sherehe hiyo, mwandishi alimtafuta Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhad Mussa Salum ambaye alionesha kushangazwa na jambo hilo na kusema ni makosa na kufanya hivyo ni kuchezea dini ya Mwenyezi Mungu.
 
“Mtu anayefanya mambo hayo ni kwamba huko ni kuchezea dini ya Mwenyezi Mungu, watu wanatakiwa kuelewa kwamba utukufu wa Mwezi wa Ramadhani ni usiku na mchana. Kama kuna staa kafanya hivyo, amemkosea sana Mungu,” alisema shehe mkuu.

Credit: Gazeti la Ijumaa/gpl
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment