Friday, July 17, 2015
Nkupamahmedia
Msanii anayekuja kwa kasi katika anga la filamu, Ester Kiama amejikuta akiangua kilio kufuatia madai yanayoenezwa kuwa ana ‘ngoma’.
Taarifa ya ‘kuungua’ kwa staa huyo zimekuwa zikisambaa kama moto wa
kifuu kwenye mitandao ya kijamii huku mwenyewe akidai anasingiziwa na
hivyo juzi kati akaamua kwenda kupima.
“Hizi
habari kwamba nina ngoma zimekuwa zikienea sana na hakuna kitu kibaya
kama kumnyooshea mwenzako kidole bila kuwa na uhakika na unachokisema.
Nakumbuka mara ya kwanza kuna mwanamke aliandika mtandaoni kuwa
nimeathirika hivyo Dude ajihadhari.
“Niliumia sana lakini ili kuwakomoa nikaenda kupima na majibu
yakaonesha niko safi, nikajikuta nalia sana, si unajua inavyouma
kusingizwa kitu? Sasa ili kuwakata kilimilimi hao wanaonizushia, majibu
haya nitayabandika mtandaoni pia,” alisema Ester.
Nkupamahmedia



0 comments :
Post a Comment