Friday, July 17, 2015
Nkupamahmedia
VIJANA takribani 30 wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), jana wamesalimisha kadi zao za CCM katika tawi la
Chadema lililopo Mwananyamala, jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa
hawakuridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea wa urais wa CCM.
Mmoja wa vijana hao akichukua kadi yake ya Chadema.
*****
Vijana hao wa vyuo vikuu mbalimbali waliokuwa wakiimba wimbo wa
tunaimani na Lowassa wamekabidhi kadi zao za CCM kwa Kaimu Mwenyekiti wa
Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni ya Chadema, Bi. Esther Semaja na kukabidhiwa
kadi za uanachama wa Chadema.
Nkupamahmedia



0 comments :
Post a Comment