
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati aliyevaa suti ya
kijivu jivu akiangalia athari iliyozikumba nyumba za Wakaazi wa Kijiji
cha Fukuchani Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya upepo mkali wa ghafla
uliovuma kwa adakika Tatu jana asubuhi. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa na Kushoto
yake ni Sheha wa Shehia ya Fukuchani Bwana Abdulla Mcha Ame.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi Mabati 1,000
yaliyotolewa na Serikali sheha wa Shehia ya Fukuchani Bwana Abdulla
Mcha Ame kwa ajili ya wananchi wa Nyuma 32 zilizathirika na Upepo Mkali.

Balozi
Seif akimkabidhi Sheha Abdulla vyakula mbali mbali kwa ajili ya
wananchi wa shehia yake waliopatwa na maafa ya nyumba zao kuezuka mapaa.
Kushoto ya Sheha Abdulla ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” Bibi Sida
Mohammed Himidi.

Baadhi
ya Nyumba za Wananchi wa Kijiji cha Fukuchani zilizokumbwa na upepo
mkali Jumatato ya Tareje Mosi Julai 2015 majira ya saa Tano za asubuhi.

Baadhi
ya Nyumba za Wananchi wa Kijiji cha Fukuchani zilizokumbwa na upepo
mkali Jumatato ya Tareje Mosi Julai 2015 majira ya saa Tano za asubuhi.

Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Kijiji cha Fukuchani zilizokumbwa na
upepo mkali Jumatato ya Tareje Mosi Julai 2015 majira ya saa Tano za
asubuhi.

Balozi
Seif akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kanal Staafu Juma Kassim
Tindwa wakiangalia moja ya nyumba zilizoezuka paa moja katika Kijiji
cha Fukuchani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Balozi Seif akimkabidhi Bwana Kidume Hamdu mchango wa shilingi 50,000/-
miongoni mwa wananchi 32 waliopata mchango huo ambao nyumba zao
zimekumbwa na upepo mkali huko Fukuchani.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa misaada kwa wananchi wake
wakati wote kwa mujibu wa hali na wakati pale wananchi hao wanapokumbwa
na matatizo au kupatwa na maafa ambayo yatahitaji nguvu ya Serikali
Kuu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli
hiyo wakati alipofanya ziara fupi ya kuangalia maafa yaliyowakumba
Wananchi wa Kijiji cha Fukuchani Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuwapa pole
baada ya Nyumba zao kuathiriwa na upepo wa ghafla Jumatano ya Tarehe
Mosi Julai majira ya saa Tano asubuhi.
Nyumba zipatazo 32 zimeathiriwa na upepo huo uliovuma kwa dakika tatu tu
ukileta mtafaruku kwa wakaazi wa Kijiji hicho cha Fukuchani pamoja na
watu waliokuwa wakisafiri kwa njia ya bara bara.
Balozi
Seif ambae aliambatana na Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Kaskazini
“A” na Mkoa wa Kaskazini Unguja aliangalia athari ya nyumba hizo ambazo
sita kati yake zimeharibika Mapaa yake, nyumba 13 maharibiko ya wastani
na nyumba 9 maharibiko madogo.
Alisema kutokana na maafa hayo Serikali imelazimika kuwafariji Wananchi
hao kwa kuwapatia msaada wa Mabati kwa kadri nyumba husika
zilivyoharibika ili kuwapa nguvu ya kuweza kuzifanyia matengenezo na
hatimae zirejee katika hali ya kawaida.
Balozi Seif aliwataka Wananchi hao wa Kijiji cha Fukuchani kuendelea
kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu kwao kwani maafa hayo
ni matokeo yasiyotarajiwa kwa vile yanatokana na maumbile ya Mwenyezi
Muungu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi wa Kijiji cha
Fukuchani kwa juhudi walizochukuwa katika kipindi kifupi katika
kuwasaidia Wananchi wenzao wakati walipokumbwa na majanga hayo.
Balozi Seif alishauri kuendelezwa kwa tabia hiyo njema ambayo kwa kiasi
kikubwa husaidia kuleta faraja kwa wale watu wanaopatwa na mitihani ya
ghafla isiyotarajiwa.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” Bibi Sida Moh’d Himid alisema
tathmini ya awali iliyofanywa na Uongozi wa Wilaya hiyo ya kuangalia
maafa hayo imeonyesha gharama iliyotokana na janga hilo ikikisiwa
kufikia shilingi za Kitanzania Milioni 92,000,000/-.
Bibi Sida alisema Uongozi huo ulilazimika kufika mara moja kwenye tukio
hilo mara baada ya kuarifiwa ili kuona jinsi gani unaweza kuchukuwa
hatua za dharura kuwahudumia Wananchi hao.
Naye Sheha wa Shehia ya Fukuchani Bwana Abdulla Mcha Ame akimkaguza
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuangakia hasara ya majengo hayo
alisema upepo huo mkubwa uliovuma ghafla haujawahi kutokea katika
Historia ya Kijiji hicho.
Sheha Abdulla alisema Dakika Tatu za kizaa zaa hicho zimesababisha
shughuli zote za kimaisha zilizokuwa zikiendelezwa na Wananachi hao
kulazimika kusimama ghafla.
Katika ziara hiyo ya kuwafariji Wananchi hao Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif alikabidhi Bati elfu 1,000 kwa Wananchi waliokumbwa
na maafa hayo, ambapo nyumba sita Kubwa zilizoezuka paa lote wakazi
wake wamekabidhiwa Bati 70 kila Mmoja.
Nyumba Tisa Ndogo ndogo zilizoezuka mapaa yake zikabahatika kukabidhiwa
Bati 30 kila nyumba na zile zilizoezuka bati chache zimekabidhiwa kwa
mujibu wa athari ilivyotokea ikiwemo Skuli ya Fukuchani ambayo imeezuka
mabati machache.
Balozi Seif pia akakabidhi mchango wake binafsi wa shilingi 50,000/- kwa
kila familia ya nyumba 32 zilizopata na athari pamoja na msaada wa
vyakula kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unaoendelea
ukiwa katika kumi la Pili ya kuachiwa huru na moto.


0 comments :
Post a Comment