Kikundi
cha ‘Mshikamano’ katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kikimsikiliza
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC BW. Muungano Saguya akiwaelezea namna
ya kukuza ujuzi na kutumia Halmashauri zao kuongeza ufanisi wa kazi
alipowatembelea nakusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili. Vijana hao
wameshapewe eneo la muda la kuendesheea shughuli zao na wameanza
kutengeneza tofali kwa ajili ya kuwauzia wanmanchi.
Hii
ndiyo hali iliyojitokeza Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Mji wa
Mpanda pale NHC ilipolazimika kuzitwaa mashine ilizotoa msaada kwa
vijana ili waweze kujiajiri. Kikundi hiki cha Mpanda Hotel ni mojawapo
ya vikundi vilivyonyang’anywa mashine Mkoani Katavi na Rukwa kwa
Halmashauri sita za Mikoa hiyo ukiacha Mlele inayofanya vizuri,
kushindwa kuzitumia mashine hizo ipasavyo. Halmashauri hizo zimetakiwa
kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara baada ya kubainika kuwa
vikundi vya awali vilundwa kisiasa.
Kikundi
cha vijana cha ITIMBA kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya
Vijijini kikimsikiliza` Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano
Kasibi Saguya alipowatembelea ili kujuwa changamoto zinazowakabili.
Kikundi hicho kimeshapata kazi za watu binafsi na shule ili kuwajengea
majengo mbalimbalia na hivyo kupata fedha za kujiendeleza. Halmashauri
ya Wilaya ya Mbeya Vijijini imekubali kuwapa vijana hao ardhi na maeneo
ya kufanyia kazi.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bw. James Milanzi
akimsikilza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya
alipofika Ofisini kwake kukumbusha wajibu wa Halmashauri za Wilaya wa
kusaidia vijana ili waweze kutengeneza matofali ya kujengea nyumba za
gharama nafuu na kujipatia ajira. Halmashauri hiyo imepiga marufuku
ukataji miti kwa ajili ya kuchoma matofali na badala yake wananchi
wametakiwa kutumia matofali rafiki wa mazingira yanayozalishwa kwa
kutumia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana katika
Halmashauri zote nchini.
Kikundi
c ha “CHAPAKAZI” Wilayani Mbarali kikiwa kinamsikiliza Meneja wa Huduma
kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea kujuwa changamoto
zinazowakabili.Halmashauri ya Mbarali imesaidia vijana vifaa na maeneo
ya kutengenezea matofali hayo na vijana wamehamasika baada ya
kuhakikishiwa soko la tofali zao.
Kikundi
cha “JITEGEMEE NA CALVARY “ Wilayani Tukuyu kikiwa tayari kumsikiliza
Meneja wa Huduma kwa Jamiii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea
ili kujuwa changamoto zinazowakabili. Kikundi hicho kimeishukuru
Halmashauri ya Wilaya ya Tukuyu kwa kuwapa eneo la kufanyia kazi na
masoko ya tofali wanazatengeneza. Kushoto ni Meneja wa NHC Mkoa wa Mbeya
Bw. Anthony Komba.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ubisimbali Jesiwande
alipokutana na timu ya NHC na kuchangia hoja ya namna ya kuondoa
changamoto za ajira zinazowakabili vijana nchini. Halmashauri hiyo
ambayo vijana wake hawajafanya vizuri imeapa kuwapa vijana wake mikopo
na kuwatafutia masoko ya matofali yao.
Kikundi
cha “Umoja wa matofali imara” Wilayani Iringa Vijijini ambacho
kimeshajenga jengo kubwa la kibiashara kwa kutumia mashine kilichopewa
msaada na NHC kilipata fursa ya kutembelewa na ujumbe kutoka NHC na
kupewa msasa na hamasa ya kuendelea kujiletea maendeleo kwa kutumia
mashine hizo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bi. Sikitu Mwemsi (kulia) akiomba timu
ya NHC iliyofanya mazungumzo naye Ofisini kwake kuwapa muda badala ya
kuwanyang’anya mashine walizopewa baada ya Halmashauri hiyo kususua
kuwasaidia vijana na kusimamia vikundi vyao. Meneja wa Huduma kwa Jamii
wa NHC ameipa Halmashauri hiyo mwezi mmoja kujiweka sawa na vijana wake
kuanza kutumia kikamilifu mashine walizopewa msaada na NHC.
Timu
ya NHC na Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo
ikiwa eneo linalotumiwa na kikundi cha vijana cha “Muungano Vijana
Kilolo”kilichopewa msaada wa mashine na NHC ambapo walikagua kazi za
vijana hao (hawapo pichani) ambapo Wilaya hiyo imeamua kuwapa mkopo
vijana hao ili wawe na benki kubwa ya matofali.
Kikundi
cha vijana cha “Umoja wa Wafyatua matofali” kilichopo katika Kata ya
Mkwawa Manispaa ya Iringa kikiwa kimeanza kazi ya kutengeneza matofali
kilipotembelewa na timu ya NHC kuona kazi zao. Hiki ni kikundi
kinachofanya vizuri katika Manispaa hiyo yenye vikundi vinne vya vijana
waliopewa msaada wa mashine na NHC za kufyatulia matofali ya
kufungamana.. UMOJA WA WAFYATULA MATOFALI MANISPAA YA IRINGA
Kikundi
cha SHIDEPHA ambacho kilipewa mafunzo ya namna ya kutumia mashine za
kutengeneza matofali ya kufungamana na NHC kikiwa imara na timu ya NHC
iliyowatembelea na kuamua kuwaongezewa uwezo kwa kupewa mafunzo na vifaa
vya kufanyia kazi. Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC baada ya kuona
juhudi zao aliamuru waongezewe mashine mbili ili wasonge mbele na
Halmashauri imekitambua kikundi hicho.
NHC
imeendelea kuwakagua vijana waliopewa msaada wa mashine za kufyatulia
matofali yatakayowezesha wananchi kujijengea nyumba za gharama nafuu
katika Halmashauri zote za Mikoa ya Katavi, Mbeya na kukamilika Mkoani
Iringa.
Kwa ujumla, vijana wana ari ya kutosha ingawa wana changamoto
zinazohitaji msukumo wa Halmashauri zao, hasa za masoko ya matofali yao
pamoja na mtaji wa kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa benki ya
matofali ya kuuzia wananchi.
Katika ziara ya NHC Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya hizo wameomba NHC
isiwanyang’anye mashine na wameahidi kuwapa vijana mikopo na kuwasaidia
malighafi za kuwawezesha kutengezea matofali hayo ikiwemo mchanga,
sementi na udongo maalum kwa kazi hiyo.
Hata hivyo, Mikoa ya Rukwa na Katavi muitikio wa vijana na Halmashauri
hizo ukiacha Halmashauri ya Mlele ambayo inafanya vizuri, umekuwa hafifu
sana na Shirika limelazimika kuzinyang’anya Halmashauri hizo mashine na
kuzitaka kuomba upya kama bado wana azma ya kutumia mashine hizo
kujiletea maendeleo ya kuwa na nyumba bora na kukuza ajira kwa vijana
wao.


0 comments :
Post a Comment