Bifu Jipya la Wema Sepetu na Aunt Ezekiel

Wednesday, July 22, 2015

Nkupamahmedia

Mafahari wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo kwenye mgahawa unaojulikana kama Snow Cream na kuchuniana kama vile hawajuani.

Kwa mujibu wa gazeti  la Risasi, Wema ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye mgahawa huo na wapambe wake kisha baada ya muda kidogo kupita, Aunt pamoja na watu wengine nao walifika na kukaa meza nyingine.

Habari zinadai kuwa baada ya Aunt kukaa, walitupiana macho na Wema bila kupeana salamu ingawa Wema hakuwahi kumuona mtoto wa Aunt tangu ajifungue.
 
Inadaiwa kuwa baada ya Aunt kumaliza kula Ice Cream na kundi lake, waliinuka na kuondoka zao na kumuacha Wema na marafiki zake.
 
Alipotafutwa  Aunt ili aweze kuzungumzia kitendo hicho na bifu lao lisema;
 
“Jamani unajua kila mtu alienda kwa ajili ya kazi zake na ndiyo kama tulivyokutana kila mmoja alikuwa yupo na taratibu zake, sioni kama ni bifu, sina comment,” .
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment