Akiongea
na waandishi wa habari leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga
ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa
michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu
nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.
Lengo
la CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza
michezo mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na
Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania
uenyeji huo na kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini
katika hali ya amani na usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano
hiyo.
Timu zilizothibtisha kushiriki michuano hiyo ni Yanga, Azam
(Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM
(Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi),
Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na
KCCA (Uganda).
Wakati
huo Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya
michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015
jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa
CECAFA.
Mechi
ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR
ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua
dimba na Telecom ya Somalia.
Ratiba ya michuano hiyo imeziweka timu hizo katika makundi matatu ambapo
kundi A lina timu za: Yanga (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Telecom
(Djbiout), KMKM (Zanzibar) na Khartoum-N (Sudan)
Kundi
B: APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi) na Heegan FC
(Somalia), Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama
City (Ethiopia) na KCCA (Uganda)
Timu
tatu zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu
kutoka kundi B & C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B
& C zitaingia katika hatua ya robo fainali.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ( katikati ) akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani ).
0 comments :
Post a Comment