KATIKA PITAPITA, TUMEPATA BARUA YA MWENYEKITI WA YANGA KUPITIA MTANDAO
WA www.manjivsmengi.com IKIELEZA MAMBO MENGI NA MWALIKO WA MDAHALO AMBAO
MANJI AMEUTOA KWA MENGI.
MDAHALO HUO UNAFANYIKA IJUMAA HII NA UTARUSHWA MOJA KWA MOJA NA TBC KUANZIA SAA 12 JIONI HADI SAA 1 USIKU. SOMA BARUA HIYO.
Hisia za Bwana Mengi kwenye vyombo vya habari kuwa kampuni yangu
inamiliki fedha za serikali chini ya Commodity Import Support (CIS)
Mengi ametupa lawama akizishutumu kampuni kama Farm Equip, Apollo Tires,
Quality Garage (sasa inaitwa QG Engineering) kuhusika na ufisadi huo wa
Sh bilioni 9.055.
YANGA ilikuwa chombo muhimu wakati wa utafutwaji wa uhuru wa nchini yetu
ya Tanganyika na baadaye Tanzania. Vikao vya Chama cha TANU ilifanyika
katika makao makuu ya klabu hii kongwe.
Vikao vilivyosaidia kuwaondoa wakoloni na kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika.
YANGA ilikuwa ni chombo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar
na ndiyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuliyonayo sasa.
Rangi tatu za Yanga ziko katika bendera ya Tanzania, sehemu ya jina lake
iko katika wimbo wa taifa, mwenge wa uhuru ni sehemu ya utambulisho wa
klabu hii.
Mwananchama namba moja wa klabu ya YANGA ni hayati Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Marehemu Mzee Karume ndiye aliyejenga
makao makuu ya klabu ya YANGA ikiwa ni sehemu ya shukurani wake katika
klabu kwa kutoa mchango mkubwa katika mapinduzi ya Zanzibar.
YANGA haimilikiwi na mtu mmoja, ni ya wanachama pamoja na Wajumbe wa
Bodi ya Wadhamini inayowajumuisha Mama wa Taifa, Mama Fatma Karume.
Wengine ni Mheshimiwa George Mkuchika ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utawala Bora, mmoja wa watu wanaoheshimika katika taifa letu.
Si viongozi pekee ambao ni mashabiki wa Yanga, hata watu wa nchi jirani
pia walipoishi hapa nchini kwa ajili ya kupambana kupata uhuru wa nchini
zao walijikuta kwenye mapenzi makubwa na Watanzania kutokana na ukarimu
wao. Kama walivutiwa na Watanzania ambao wengi ni mashabiki wa Yanga,
hili halina ubishi na kwa kuwa mimi ni Mwenyekiti wa Yanga, nawatakia
kila la kheri popote walipo.
Mimi ni Yusuf Mehbub Manji (39), Mwenyekiti kijana zaidi kutoka katika klabu ya Yanga.
Nilichaguliwa Julai 14, 2012 kwa ushindi wa 97.5%. Inapofikia hatua
mwenyekiti wa klabu kubwa na kongwe kama YANGA kuitwa ni mwizi, fisadi
na mla rushwa na kadhalika inanifanya nifikie uamuzi wa aina mbili.
Moja ni kuachia ngazi au nichukue uamuzi wa pili wa kujibu kwa
Wanayanga, Watanzania na Afrika nzima. Kwani kukaa kimya ni kuleta
maumivu na dharau kubwa kwa klabu hii kongwe na watu wake ambayo kazi
yake kubwa ni kuwapa furaha Wanayanga na wapenda michezo.
Katika taarifa iliyoandikwa katika gazeti la NIPASHE la Juni 8, 2015
lililo chini ya IPP Media, inayomilikiwa na Bw. Reginald Abraham Mengi,
inaeleza kuwa Kampuni zangu (limezitaja Farm Equip Tanzania and Quality
Garage ) zimefanya ufisadi kwa serikali ya Tanzania unaofikia Sh bilioni 9.055 chini ya Commodity Import Support.
Taarifa hiyo ilitoka katika vyombo vya habari vya Bw. Mengi pekee.
Ukweli ni kwamba habari hizo ni uongo mtupu, tena wa kupindukia
kuhusiana name unaonezwa na vyombo hivyo vya habari vya Bw Mengi.
Mwenyekiti wa YANGA si fisadi, mwizi, mungo kama ambavyo taarifa
zinazosambazwa na vyombo hivyo vya habari vya adui namba moja wa klabu
ya Yanga Reginald Abraham Mengi.
Mwenyekiti huyu wa YANGA kamwe hapokei mshahara wala posho yoyote kutoka
klabu. Hapati faida yoyote ya kifedha zaidi ya kuwa zawadi ya aina yake
na kipekee kwa wengine na kuwa mtu anayeweza kuwapa furaha wengine.
Zawadi hiyo aliyonayo mwenyekiti wa YANGA ni furaha ya wengi hasa pale
timu inapofanya vizuri kwa kushinda mechi zake na makombe na kuwapa
mamilioni furaha ya moyo na kuwafanya wasahau matatizo yao na ndiyo
furaha na malipo yangu.
Kwa wale ambao wanaweza kumkumbuka Mengi, alijaribu kutaka kuingoza
Yanga katika miaka ya 1990 lakini wazee walimfukuza. Hii ilikuwa ni
baada ya kugundua alikuwa akichochea migogoro ili aweze kuingoza Yanga
kwa maslahi yake binafsi.
Wakati wa mkutano wa wanachama uliofanyika katika Hoteli ya Starlight na
Bw Mengi kulazimika kujificha chooni baada ya walinzi wake binafsi
kuzidiwa na hasira za wanachama. Nakumbuka mwanachama mmoja alimueleza
hivi: …” ungeenda kwanza kumaliza matatizo ya ndoa yako kuliko
kuendeleza mgogoro katika klabu yetu (kweli mgogoro ambao aliutengeneza
kwa makusudi).” Baada ya siku hiyo kufanikiwa kuokolewa na Polisi,
hakuwahi tena kurejea Yanga.
Mwanzoni mwa 2006, wakati ndiyo nikiwa na umri wa miaka 36, niliombwa
kuingia kuisaidia klabu ambayo ilikuwa katika hali mbaya kifedha. Kwamba
niwe mdhamini mkuu na siku chache baadaye taarifa zilimfikia Bw Mengi
ambaye alionekana kutofurahia na Machi 26 alianza kutumia magazeti yake
kunishambulia kwa nia ya kunichafua kwamba mimi ni mhalifu, muongo na
fisadi.
Kwa kuwa nilikuwa ni mwananchi wa kawaida, si kiongozi wa klabu kubwa
kama Yanga, niliamua kutafuta haki yangu kwa kumfungulia kesi
mahakamani. Kesi ambayo nilishinda na yeye kutakiwa kunilipa Shilingi 1.
Nilipohoji uwezo wa kufikiri, kutafakari na kuamua wa mengi, aliamua
kunifungulia kesi akidai nimlipe Sh bilioni 150, mwisho alishindwa na
sasa anatakiwa kulipa kiasi cha Sh bilioni 5 kwa uendeshaji wa kesi.
Nawakumbusha kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Bw Mengi alifungua kesi
kesi mbili, moja akipoteza na nyingine alimua kujitoa au kuifuta
mwenyewe. Hii inaonyesha kiasi gani kumekuwa na ukweli katika yale
ambayo nimekuwa nikimueleza.
Kabla sijachaguliwa kuwa mwenyekiti wa YANGA mlinijua, mlijua nilikuwa
mtu ninayekipigania ninachokiamini na kama nilikiamini kitu, basi
ilikuwa ni njia yangu sahihi ya kushinda.
Najua kwa wanachama wa Yanga wamekuwa wakiona namna Mengi
anavyonishambulia katika vyombo vyake vya habari lakini wamekuwa
wakipuuzia na kunipa heshima yangu kama mtu niliomaliza mgogoro mkubwa
na mgawanyiko ndani ya klabu ya Yanga ambao niliumaliza ndani ya miezi
mitatu tu baada ya kuwa mdhamini mkuu wa klabu.
Niliunda bodi ya kwanza ya wadhamini kwa kuwaomba wazee waanzishe baraza
lao. Halafu mimi nilijiuzulu kwa kuwa nilikua ni kijana mno, miaka 33
nisingefaa kuwa mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini. Mwisho nikaaga
kwa kuwa kazi yangu ilikuwa imekwisha.
Wazee wa Yanga waliamua kufanya dua maalum kwa ajili yangu, wakanisimika
na kunifanya kuwa CHIFU wa kwanza wa klabu kwa kunipa ngao yenye nembo
ya klabu pamoja na mkuki.
Nilipotakiwa kwa mara nyingine katika klabu, nikiwa na miaka 36
nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu kongwe ya YANGA.Kitu ambacho
najivunia kwa kuwa kiongozi kwani hata familia yangu imekuwa ikipata
heshima kutoka kwa wanachama na mashabiki wa Yanga.
Wakati mwingine mama yangu anapokwenda sokoni, wakati mwingine hatakiwi
hata kulipa kutokana na heshima ya kuwa mama wa Mwenyekiti wa Klabu
yenye heshima ya YANGA. Mmenipa heshima kubwa, mfano watoto wangu
katika akaunti zao za Facebook hawawezi hata kuweka picha yangu kwa hofu
ya kupata marafiki wengi kupindukia.
Mke wangi analazimika hata kutumia jina tofauti kwa kuwa mapenzi makubwa
anayopata kutoka kwa mashabiki wa klabu ya YANGA yanafikia hadi kumpa
hofu na hii ni kwa kuwa wanachama na mashabiki wanajua huyu ni mke wa
mwenyekiti wao ambaye wanamuamini na kumpenda sana.
Kwa mapenzi haya ninayopata ninaahidi nitaendelea kufanya kila
ninaloweza kwa uwezo wangu wa juu, hali na mali kwa klabu katika kipindi
changu chote wakati nikiwa mwenyekiti. Mapambano yanaendelea kwa ajili
ya klabu yetu.
Tokea Bw Mengi alipofukuzwa na wanachama wa YANGA, amekuwa mwoga
kuhusiana na maisha yake, amejaa hofu akidhani kuwa kila Mtanzania
anataka kumuua! Anaomba ulinzi wa Jeshi la Polisi huku akiwa hajui
asilimia kubwa ya askari Polisi nao ni YANGA.
Nashangaa alitaka Yanga iharibikiwe kabisa, lakini yeye ndiye
anayekimbilia katika runinga akidai kuna watu wanatanga kumuua. Bw
Mengi, YANGA haitaki kukuua, lakini tunakuchukia ingawa tumekuwa
wastaarabu na tunajizuia. YANGA tunachotaka ni wewe kutuacha tuendelee
na maisha yetu na familia yetu, endelea na yako.
Tungependa hata usizungumzie jina la klabu yetu kupitia kalamu yako wala midomo yako.
Lakini inaonekana kama shetani, umekuwa ukijaribu kurejea katika klabu
ya YANGA tena ukionyesha umepania kutufelisha kitu ambacho kamwe hauwezi
kufanikiwa hata kidogo. Hauwezi ukashinda uimara wa mioyo yetu ambayo
imeunganika na kuwa kitu kimoja. Unaonekana unataka kutumia nafasi hii
kurejea na kuomba msamaha kwa mabaya ulioifanyia klabu.
Kama kweli sisi Watanzania tunajulikana dunia nzima kama ni watu
tunaoishi kwa amani, watu wenye upendo na wakarimu kwa nini kila mwaka
unalalamika kuwa kuna watu wanataka kukua? Au ndiyo ndoto mbaya
zinakuandama kutokana na mabaya uliyoyafanya huko nyuma, hivyo unataka
kuomba msamaha?
Bw Mengi, mimi sihitaji kulilia ulinzi kama unaotaka wewe. Ulinzi wangu
ni mamilioni ya Wanayanga waliopo. Sihitaji fedha ninapotembea sehemu
yoyote ya Tanzania kwa kuwa hakuna Mwanayanga anayehitaji fedha kutoka
kwangu.
Sihitaji tuzo yoyote ili nijulikane au matangazo ili wanijue, hakuna
Mtanzania asiyenijua. Pia sihitaji pasi ya kusafiria ya kibalozi
ninapokuwa uwanja wa ndege. Kama ni heshima ya red carpet, basi
ninaipata kwa kuwa Mwenyekiti wa Yanga ambaye ni mkweli na muwazi.
Ntaendelea kuwa mwenyekiti mwaminifu ninayejitolea kwa uwezo wangu wote
kwa klabu ninayoingoza, kama siku itafikia kifo. Basi nitakuwa na
uhakika watoto na familia yangu itakuwa katika mikono salama ya
wanachama na mashabiki wa YANGA ambao wamesambaa dunia nzima.
Bw Mengi, mimi ni mtu wa kawaida tu niliyelelewa na baba ambaye wakati
wa vita ya kumng’oa Nduli Iddi Amini Dada alitengeneza bodi ya gari
maalum kwa ajili ya wanajeshi wa Tanzania waliokwenda kupambana ambao
baadaye walimshukuru kwa kutembelea sehemu aliyokuwa akitumia
kutengenezea mabodi hayo.
Tokea hapo, kila Rais alitembelea katika gereji yake hiyo ndogo.
Nilifunga ndoa mwaka 1994, ilihudhuriwa na wageni kama Mheshimiwa Rais
Ali Hassan Mwinyi, Marehemu aliyekuwa Wazidi Mkuu, Cleopa Msuya,
Mheshimiwa John Malachela na viongozi wengi wakubwa. Sasa nina watoto
wawili wa kiume, mmoja akiwa na umri wa miaka 17 na mwingine 12.
Nakuuliza, ulikuwa wapi wakati wa vita vya Kagera pia ndoa yako ya sasa ina umri gani?
Haujawahi kuchaguliwa hata kuwa myampara tu wa gereza, lakini ajabu unajidanganya mwenyewe eti ni kiongozi bora.
Tunajua haukufurahia Yanga kushinda taji lake la 25 la Ligi Kuu Bara
msimu uliopita! Kumbuka Mataji 50 tu ymegombewa, hivyo Yanga imebeba
nusu ya hayo hadi sasa. Haufurahii kuona kijana mdogo kama mimi napendwa
na watu wengi kuliko wewe, ndiyo maana umekuwa ukiamua kujipamba kama
vile vitabu vya ujanjaujanja kwamba wewe ni kati ya watu matajiri zaidi
Tannzania!
Mtu usiye na huruma kuamua kupitia viwanda vyako kuchanganya dawa kutoka
Marekani na maji ya Tanzania na kuyaita Coca-Cola, kuchanganya kalamu
na karatasi na kuita taarifa! Kujionyesha wewe mwenyewe kwenye runinga
yako, halafu unataka watu waamini hiyo ni taarifa kwao!
Unawalazimisha wanasiasa wakuombe ardhi au migodi ili uiendeleze wakati
hauna mtaji wa kufanya hivyo! Waliogundua kuwa huna uwezo huo
unawashambulia kwa madai wamewapa wageni na ungepewa wewe migodi ya gesi
ungeweza kutuwasaidia sisi Watanzania masikini.
Kama sikosei thamani yako ni dola milioni 550, unapata faida ya 10%.
Mfano dola milioni 55 utatakiwa kulipa kodi ambayo itakuwa si chini ya
dola milioni 16.5 kwa mwaka. Je, umekuwa ukilipa kodi hiyo? Mimi kama
Mwenyekiti wa Yanga najua kila kitu kuhusiana na wewe.
Bw Mengi, usitake kudanganya watu biashara uliyoanzisha miaka 10
iliyopita eti thamani yake sasa ni dola milioni 550. IPP ilianzishwa
mwaka 1981, kabla ya hapo ulikuwa mhasibu tu. Nauliza, unafikiri YANGA
hawajui kuhusiana na uhusiano wako kwao hadi walipofikia kuniongezea
muda kama mwenyekiti wao. Wanajua thamani yangu kuliko wewe na uhasibu
wako.
Ninaweza nikakupa mfano wa biashara zangu, lengo si kujigamba. Sitaki
kuzungumzia kampuni kubwa ya uvuvi katika Ziwa Victoria au kampuni kubwa
ya Rice Mill ya Morogoro. Nitakupa mfano mmoja tu, Novemba 25, 2011
nilifungua maduka makubwa ya biashara na mmoja wa wanasiasa wakubwa
barani Afrika ambaye sasa ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Mheshimiwa
Railla Odinga ndiye alikuja kuyafungua akiwa mgeni rasmi na mwalikwa
siku hiyo. Wewe umefungua biashara gani kubwa ndani ya miaka 10 na
kiongozi yoyote wa Tanzania akaja kuizindua?
Maisha yangu nimekuwa mjumbe wa bodi ya Afrika ya kupambana na ugonjwa
wa ebola maarufu kama African Union Ebola Solidarity Trust Fund ambako
nimesaidia kupatikana kwa fungu la dola milioni 50 kupambana na ugonjwa
huo hatari na kuutokomeza kabisa kwa wale ambao waliobaki wameathirika
katika nchi ya Sierra Leone.
Angalia mashabiki na wanachama wa Yanga katika mitandao wanavyoonekana
wakiwa wameungana na wenye furaha kubwa kushangilia ushindi au ubingwa,
hii inahamasisha hata vijana. Kwa miaka 10 nimefanya makubwa kwa bara
letu la Afrika, ajabu unaona si sahihi, umeamua kufanya ujanja ujanja
kwa kununua tuzo. Najaribu kujiuliza watu wangapi watakuja katika
mazishi yako kama itakavyokuwa kwangu, kijana uliyejaribu kutaka
kumharibia tokea akiwa na miaka 30, huku ukijaribu kuniharibia biashara
zangu.
Lakini Mungu ni mwema, ameamua kunichagua kuwa mmoja wa vijana wanaopendwa zaidi nchini Tanzania kama si Afrika kote.
Bw Mengi, umekuwa na tabia ya kuwachafua watu kila unaposhindwa kupata
unachotaka kwamba ni wala rushwa na mafisadi! Mahakama Kuu ya Uingereza
ambayo ulifungua kesi kwa madai ya kuitwa muongo na maneno mengi,
imetupa kesi yako kwa kuonekana haikuwa na mantiki. Sasa uamuzi
umekugeukia kwamba si muongozo tu au si mwaminifu tu lakini imeonekana
ni mtakatishaji wa fedha, vyombo vyako vya habari havifuati weledi,
badala yake vinafuata wewe unafuata au kufadika na kipi!
Inaonekana IPP hakuna uhuru wa habari na waandishi wenyewe isipokuwa
kile unachotaka wewe hadi kufananishwa na ujasusi wa habari (sawa na ule
wa Osama Bin Laden wa Al-Quaeda au ISIS kwa siku za karibu).
Kesi hiyo imekugeukia kwamba kwa sharia za Tanzania unapaswa kushitakiwa kwa jinai na vyombo vya sharia vya Tanzania.
Kwa nafasi ya Mwenyekiti wa YANGA na kama mwangalizi mkuu, nitapambana
kulinda jina la klabu hii tukufu na kama Mwenyekiti wa YANGA ningependa
kutangaza kumualika Bw Mengi katika mdahalo utakaorushwa na runinga moja
kwa moja Ijumaa ya Julai 3, 2015.
Watanzania watakuwa na nafasi ya kuulizwa maswali katika mdahalo huo wa
wazi na moja kwa moja. Hii itakuwa nafasi nzuri kwa Bw Mengi kuja au
kutoa ushahidi wake kuhusiana na ufisadi wangu kwa uthibitisho. Pia
utakuwa wakati mzuri kwa Watanzania kujua nani ni mkweli na yupi hayuko
sahihi.
Pia ningependa Watanzania wapewe nafasi ta kupiga kura kwa ujumbe mfupi
wa simu (SMS) kama kweli wameona mimi ni fisadi. Kama itakuwa hivyo,
basi nitajiuzulu mara moja uenyekiti wa YANGA.
Ni jukumu langu kama Mwenyekiti wa Yanga kumaliza upuuzi huu ambao
unaozushwa na Bw Mengi ambao unaweza kuiondoa klabu yetu katika utulivu
na kuweza kufanya mambo yake kwa mpangilio mzuri kama ambavyo tumekuwa
tukitaka. Yanga imekuwa ikiwavutia wachezaji wengi wakiwemo wa
kimataifa, pia tuko katika harakati za kuhakikisha tunajenga uwanja wetu
wenyewe na YANGA yenye mipango endelevu na thabiti.
Sioni kama kuna sababu ya kupoteza muda wangu wa kuitumikia Yanga kwa
ajili ya mtu anayewalaghai watu kuwa yeye ni mtu mzuri, mwema, kitu
ambacho ni uongo mtupu. Nasisitiza, sasa imetosha.
Ukweli utajulikana hiyo Julai 3, 2015 na kama Bw Mengi atakuwa na ukweli
anaotaka kuuweka wazi, basi hatasita au kukimbia kuja kukaa name mbele
ya Watanzania kwenye mdahalo. Lengo ni kumaliza ubabaishaji huu na
ugaidi kupitia vyombo vyake vya habari kwa kuwa nimechoka sasa na hali
hii kwa kuwa inanichosha na kuchukua nguvu zangu za kupambana na
maendeleo ya klabu.
Klabu ya Yanga ni tukufu katika nchi, uongo wa Bw Mengi umekuwa ukifanya
hata baadhi ya wanaotaka kufanya biashara na klabu, mashabiki au
wanachama kuingoa hofu kwamba klabu yetu inaendeshwa na fedha chafu,
jambo ambalo si sahihi hata kidogo.
Yanga Daima Mbele, Nyuma Mwiko. Ndiyo maana nataka huu mdahalo ili
kumaliza maneno yasiyokuwa na ukweli ya Bw Mengi kwa miaka takribani 20
sasa. Tunataka kumaliza hilo ili tuelekeze nguvu zetu kwenye maendeleo
ya klabu na kuachana na Bw Mengi ambaye amekuwa akitumia vyombo vyake
vya habari kutaka kutuvuruga kwa makusudi.
Acha nihitimishe hili; kuwa mwisho lazima tujue ni mimi mbaya kwa
Tanzania au Bw Mengi, kiongozi huyu ambaye alitaka kura za Wanayanga
lakini sasa yuko ofisini akifanya kila analoweza kuivuruga Yanga huku
akihakikisha tunashindwa katika kila jema na bora tunalotaka kufanya kwa
ajili ya klabu yetu. Waanzilishi wa klabu yetu, taifa na viongozi
tutakuwa na kila sababu ya kujilaumu wenyewe kama tutashindwa kufikia
malengo na tunachokitaka kwa ajili ya klabu yetu.
MUNGU IBARIKI YANGA, TANZANIA NA AFRIKA.
NINAWASHUKURU SANA.
Yusufali Mehbub Manji
(Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga)
SOURCE: http://www.manjivsmengi.com/
0 comments :
Post a Comment