Staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido.
STAA wa
muziki kutoka Nigeria, Davido ameweka wazi kuwa ana mpango wa kuimba
wimbo kwa kushirikiana na Ali Kiba na mchakato unaendelea kimyakimya.(P.T)
Ali Kiba.
Davido
ambaye jina lake lilipata umaarufu nchini kutokana na kushirikiana na
Diamond katika Wimbo wa Number One Remix, aliweka wazi hayo wakati
akipita kwenye ‘red carpet’ kwenye usiku wa Tuzo za MTV Mama, wikiendi
iliyopita.
“Tanzania ni nyumbani kwangu baada ya Nigeria, napapenda tangu siku ya kwanza nilipofika, nitafanya kazi pia na Ali Kiba, naamini itakuwa bomba, watu wasubiri tu,” alisema Davido bila kufafanua zaidi.

0 comments :
Post a Comment