
Mkutano kati ya Lowassa na vyombo vya habari, unalenga kumshitaki
Kikwete kwa wananchi kwa kile kinachoitwa, “kukaidi matakwa ya wengi.”
Lowassa alikuwa miongoni mwa wanachama 38 wa chama hicho waliojitosa
katika mbizo za urais, lakini jina lake liliondolewa katika hatua za
awali. Kikwete ndiye anayetajwa kumuengua Lowassa kwa maslahi yake
binafsi.
“Ni kweli kwamba Edo (Edward Lowassa), amepanga kueleza kilichotokea
Dodoma kwenye mikutano ya chama chake. Atafanya hivyo kupitia mkutano
kati yake na waandishi wa habari,” ameeleza mmoja wa watu waliokaribu na
kiongozi huyo.
Hakuweza kufahamika mara moja, ikiwa Lowassa atautumia mkutano huo kueleza mustakabali wake wa baadaye wa kisiasa.
Chanzo:Mwanahalisi Online


0 comments :
Post a Comment