Waziri
mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Ndugu Edward Lowassa leo
amekaribishwa rasmi kujiunga na Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA).
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari kwenye Makao Makuu ya Chama Cha
Wananchi (CUF) Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia amesema
‘tumemkaribisha Mh Lowassa kujiunga na UKAWA ili kuongeza nguvu ya
kuhakikisha tunaitoa CCM madarakani kwani tunaamini Mh Lowassa ana uwezo
wa kuhamasisha umma kuitoa CCM Madarakani katika uchaguzi mkuu ujao’.
Mkutano huo umehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu
Lipumba na Mwenyekiti wa NLD Mh Emmanuel Makaidi.
Viongozi
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA wakinyanyua juu mikono kama ishara
ya mshikamano katika kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.




0 comments :
Post a Comment