MAHAKAMA Kuu ya Tanzania YAKANA RUSHWA

indexNA MWANDISHI WETU
……………………………………..
MAHAKAMA Kuu  ya Tanzania imewataka wananchi  wenye malalamiko kuhusu vitendo vya rushwa  mahakamani kutoa ushirikiano ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Hayo yalisemwa katika taarifa  kwa vyombo vya habari  iliyotolewa leo jijini Dar es salaam  na   Afisa Habari  Mary Gwera wa Mahakama hiyo kufuatia gazeti moja la hapa nchini la Julai 21 mwaka huu  kupitia makala yenye kichwa cha habari  “Mtandao wa rushwa Mahakamani huu hapa” .
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, baada ya kufanya uchunguzi juu ya  kesi  zilizoandikwa katika makala hiyo Mahakama haikuweza kupata maelezo sahihi  kuhusu kesi   mbalimbali  za watu  wenye malalamiko hayo ambao ni Muhidini Nguluma ,Kuruthum Majjid, Abadallah Majata, Halima  Abdan, Claudiana  Mbazigwa Mpondela na  Laizer Kaanan.
“Ili kuondoa  kero  zilizobainishwa katika gazeti la Mwananchi , mahakama inatoa  rai  kwa gazeti  la Mwananchi  au mtu yoyote  mwenye taarifa sahihi  kuipatia ushirikiano ili kupata namba za simu za kesi zilizolalamikiwa  na mahakama zilikofunguliwa,” ilisema taarifa hiyo.
 Aidha mahakama hiyo imeomba wale wote waliotajwa katika makala hiyo wafike Makao Makuu ya Mahakama, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Namba 11409 Kivukoni Front waonane na Mkurugenzi Msaidizi wa Malalamiko katika Idara ya Ukaguzi wa Huduma za Mahakama na Maadili ili watatuliwe kero zao.
Mahakama hiyo inasisitiza kwamba imeweka namba za simu 0752–500 400. mitandao ya kijamii,  WhatsApp, na barua pepe info@judiciary. go.tz) ili wananchi na wadau mbalimbali  waweze kutoa malalamiko yao, maoni na mapendekezo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment