@nkupamah blog
Mwenyekiti wa Mtandao wa
Wajasiriamali Wadogowadogo Tanzania (MWATA) Bibi. Magdalena Kalani
akisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa Karakana ya wajasiriamali
wadogowadogo na uzinduzi wa mradi wa Kijani Kibichi mapema wikiendi hii
jijini Dar es Salaam. Mwenye nguo nyekundu ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Bibi. Sophia Mjema na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO
Mhandisi Omary Bakari.
Picha na Frank Shija, WHVUM
Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa
Wajasiriamali Wadogowadogo Tanzania (MWATA) Bw. Adam Ngamange
akizungumza na wajasiriamali wadogowadogo waliohudhuria hafla ya
uzinduzi wa mradi wa Kijani Kibichi mapema wikiendi hii jijini Dar es
Salaam. Mradi huu wa unalengo la kuwaunganisha pamoja wakulima wa
mbogamboga na matunda pamoja wafugaji wepesi wanaofuga wanyama na ndege
kama vile Sungura, Kwale na Samaki.
Baadhi ya wadau wa Kijani Kibichi
walioshiriki katika karakana iliyowakutanisha wajasiriamali wa
mbogamboga na matunda wakifuatilia uzinduzi wa mradi huo mapema wikiendi
hii.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi.
Sophia Mjema akionyesha fomu za kujiunga na Mtandao wa Wajasiriamali
wadogowadogo Tanzania (MWATA) ambapo alikabidhiwa fomu mbili moja
kwaajili ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kijani Kibichi mapema wikiendi hii
jijini Dar es Salaam. Mradi huu wa unalengo la kuwaunganisha pamoja
wakulima wa mbogamboga na matunda pamoja wafugaji wepesi wanaofuga
wanyama na ndege kama vile Sungura, Kwale na Samaki.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi.
Sophia Mjema akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali
mmoja ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mtandao wa
Wajasiriamali wadogowadogo Tanzania (MWATA) mara baada ya kuzindua mradi
wa Kijani Kibichi mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam. Mradi huu
unalengo la kuwaunganisha pamoja wakulima wa mbogamboga na matunda
pamoja wafugaji wepesi wanaofuga wanyama na ndege kama vile Sungura,
Kwale na Samaki.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi.
Sophia Mjema ( mwenye nguo nyekundu) akiangalia bidhaa za wajasiriamali
wa mbogamboga wakati wa uzinduzi wa mradi wa Kijani Kibichi unaratibiwa
chini ya Mtandao wa Wajasiriamali wadogowadogo Tanzania (MWATA) mapema
wikiendi hii. alikabidhiwa fomu mbili moja kwaajili ya Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Said Mecky Sadick aliyewakilishwa na mku wa wilaya huyo
katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kijani Kibichi mapema wikiendi hii
jijini Dar es Salaam. Mradi huu wa unalengo la kuwaunganisha pamoja
wakulima wa mbogamboga na matunda pamoja wafugaji wepesi wanofuga
wanyama na ndege kama vile Sungura, Kwale na Samaki.
……………………………………………………………………….
Na: Frank Shija, WHVUM
Wajasiriamali wadogowadogo washauriwa kujiunga katika vikundi
ili kuongeza nguvu ya pamoja katika uzalishaji na utafutaji wa masoko
kwa pamoja.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi. Sophia Mjema alipokuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Mecky Sadick katika Karakana iliyoandaliwa na Mtandao wa Wajasiriamali wadogowadogo Tanzania (MWATA) ambapo iliambatana sambamba na zoezi la uzinduzi wa mradi wa Kijani Kibichi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu huyo wa Wilaya alisemakuwa ni vyema vijana wakajiunga katika makundi madogomadogo ya wajasiriamali ili kuunganisha nguvu katika kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye viwango na kukidhi hitaji la soko.
Aidha aliupongeza Mtandao wa wajasiriamali wadogowadogo Tanzania (MWATA) kwa kubuni mradi utakaowaunganisha wakulima wakulima wadogowadogo na kuongeza kuwa kupitia mradi huo ni imani yake kuwa nhci itanufaika ikiwemo kuongeza uhakika wa kipato na kuimarika kwa afya za watanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Wajasiriamali Wadogowadogo Tanzania (MWATA) Bibi. Magdalena Kalani alisema kuwa wameamua kubuni mradi huo ili kuongeza tija kwa wakulima wa mazoa ya mbogamboga na matunda pamoja na ufugaji mwepesi ili kukidhi ubora na upatikanaji wa soko la uhakika
Magdalena amesema kuwa kupitia mradi huo wajasiriamali watapata fursa ya kupata huduma kutoka kwa wadau muhimu katika sekta ya uzalishaji mali ambapo aliwataja wadau hao kuwa ni pamoja na SIDO, TBS,NSSF,SAGCOT, GSI, TANTRADE na wengine wengi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Mhandisi Omary Bakari akitoa salama kutoka SIDO alisema kuwa wajasiriamali iliwafanikiwe ni vyema wakashirikiana na taasisi yake ili kuweza kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango stahiki ili waweze kuendana na ushindani wa soko ndani na nje ya nchi.
Mradi wa Kijani kibichi ni mradi unaoratibiwa na Mtandao wa Wajasiriamali Wadogowadogo Tanzania (MWATA) ambapo lengo lake ni kuwaunganisha wakulima wa mbogamboga na matunda nchini kote ili kuleta hari ya uzalishaji wenye tija na kupitia kilimo hai.Mpaka sasa mradi huu unatekelezwa katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Geita, Dar es Salaam, Kigoma na Katavi

0 comments :
Post a Comment