…………………………………
Mabadiliko katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini yamepelekea kuwepo na mabadiliko ya sheria ya mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF). Sheria ya Mfuko wa pensheni wa PSPF sasa inaruhusu kusajili wanachama katika sekta zote za umma na binafsi. Na kwa sasa mfuko una mipango miwili ya uchangiaji wa lazima yaani PSPF Mandatory Scheme na mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSPF Supplementary Scheme
Mabadiliko katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini yamepelekea kuwepo na mabadiliko ya sheria ya mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF). Sheria ya Mfuko wa pensheni wa PSPF sasa inaruhusu kusajili wanachama katika sekta zote za umma na binafsi. Na kwa sasa mfuko una mipango miwili ya uchangiaji wa lazima yaani PSPF Mandatory Scheme na mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSPF Supplementary Scheme
Akizungumza katika mahojiano
maalum na Mwandishi wa Makala hayaBi Mwanjaa Sembe, Meneja Mpangowa
Uchangiaji wa Hiari PSPF anasema uwasilishaji michango kwa kutumia
huduma ya MaxMalipo itawasaidia wachangiaji kupata huduma za michango
yao.
Anasema huduma ya kulipia kupitia
mfumo wa Maxmalipo imeanzishwa na mfuko wa pensheni wa PSPF kwa ajili ya
kupanua wigo kwa wanachama wa mfuko huo kuchangia na kujua salio la
michango yao popote walipo ambapo huduma hiyo itawarahisishia watumiaji
kutosafiri kwa umbali mrefu ili kupata huduma hiyo.
Mfuko umeona adha na shida
walizokuwa wanazipata wateja wetu ndio maana tukaamua pamoja na huduma
nyingine zitolewazo na mfuko wetu tujiunge na wenzetu wa Kampuni ya
MaxCom inayotoa huduma ya Max Malipo ili kuweza kuwakomboa wateja waweze
kuchangia pamoja na kujua kiasi cha michango yao kwa urahisi kwa
kutumia huduma hiyo hivyo kuwafanya kuwa na muda mrefu wa kutafuta
kipato badala ya kusafiri kwa umbali mrefu kufuata huduma.Anasema Bi.
Sembe.
Anasema masuala ya hifadhi ya
jamii yanagusa kiini muhimu sana cha wafanyakazi kwenye sekta rasmi na
sekta zisizo rasmi hasa za watu masikini pamoja na sekta ya bima za
jumuiya za waajiri.
Uchunguzi unaonyesha kuwaIdadi
kubwa ya watu waliomo katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii ni wale
ambao wameajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi. Hifadhi ya jamii ni haki ya
kila mtu ndiyo maana mfuko wa pensheni wa PSPF wana mpango wa uanachama
wa hiari kama mkakati wa makusudi juu ya kupanua wigo wa hifadhi ya
jamii ili kuhakikisha ya kuwa hata wale waliojiajiri kujiunga na mfuko
wa PSPF na hata wale wanachama wa mifuko mingine iliyopo kuweza kuweka
akiba ya ziada.
Hili ni jambo ambalo liko wazi
kabisa ya kwamba kila binadamu ana uhusiano mkubwa na hifadhi ya jamii
iwe kinadharia au kivitendo kutoka kuzaliwa kwake mpaka kufa, binadamu
mwenyewe lazima ajishughulishe na kazi hatarishi na kuugua magojwa
mbalimbali hivyo binadamu lazima akumbane na majanga mbalimbali kama
vile majanga ya kiuchumi na ya kijamii yanayosababishwa na kukoma au
kupungua kipato kutokana na maradhi, kujifungua, ukosefu wa ajira,
ulemavu, uzee, kifo na kuongezeka kwa gharama za matibabu.
Majanga yote ni matukio ya kila
siku kwa binadamu ambayo hayatabiriki na yote yanaaangukia kwenye mpango
wa hifadhi ya jamii. Hivyo ni kitu cha asili ya kwamba kila mtu lazima
ajue hifadhi ya jamii ni nini kwa sababu ni sehemu ya maisha ya
mwanadamu.
Bi Matilda Nyallu Meneja Msaidizi
wa Mfuko wa Uchangiaji wa Hiari kutoka PSPF anasema aina za mafao
yanayotolewa na mpango huo wa hiari ni kama vile fao la uzeeni, fao la
kifo, fao la elimu, fao la ujasiriamali , fao la ugonjwa/ulemavu, na fao
la kujitoa.
Anasema mtu yeyote aliyejiajiri,
mkulima, mvuvi, mfanyakazi wa ndani, wafanyabiashara wadogo wanaweza
kujiandikisha kwa hiari na kulipa kadri ya uwezo wake wa kipato kwenye
mfuko wa pensheni wa PSPF.
“Uchangiaji katika mpango huu wa
hiari wa PSPF Wanachama wana uhuru wa kuchagua jinsi ambavyo wanaweza
kuwasilisha michango yao, iwapo ni kwa siku, wiki, Mwezi au kwa msimu
kutegemea na upatikanaji wa kipato cha mwanachama.Michango huwasilishwa
moja kwa moja kupitia akaunti za benki au wakala wa Maxmalipo, M-pesa,
Tigo-pesa na Airtel money, ambapo kiwango cha uchangiaji ni kuanzia
shilingi 10,000 za kitanzania au zaidi” Anasema Bi Matilda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo
Bwana Adam Mayingu anasema makubaliano waliyoyafikia na Kampuni ya
MaxCom yatasaidia PSPF kutumia mtandao wa mawakala hao kutoa huduma
kirahisi
‘Sasa wateja wetu wanaweza kutumia
mawakala wa Maxmalipo waliopo kote nchini kuchangia michango yao ikiwa
ni pamoja na kupata risiti na kujua kiwango chake anachochangia kwa muda
wowote pasipo kusafiri kwa umbali mrefu.’.Anasema Bw. Mayingu.
Anasema kwa sasa dunia imekuwa
kijiji na PSPF imekuwa ikiendana na mabadiliko yanayoendelea popote
ulimwenguni ili kuweza kukidhi kiu na matarajio ya wateja wao ikiwa ni
pamoja na soko la ushindani wa kibiashara.
Katika mahojiano na mwandishi wa
malaka haya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Maxcom Tanzania Juma
Rajabu anasema huduma ya Maxmalipo ni rafiki na rahisi kutumia kwa
watumiaji na imeenea nchini kote hivyo itawarahisihia na kuboresha
utendaji kazi wa PSPF.
Unajua sasa hivi mtandao ndio kila
kitu katika ulimwengu wa biashara, watu hawana muda wa kupotezaau
kusafiri kwa umbali mrefu wanataka kufanya jambo la haraka na lenye
uhakika na kuendelea na shughuli nyingine za uzalishaji mali na
kuchangia katika kipato chao na nchi kwa ujumla, haya ndio mabadiliko
yanayoendelea kwa kasi zaidi duniani kote, Anasema Bwana Rajabu.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Juma Nkamia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi wa huduma hiyo anasema kuanzishwa kwa huduma hiyo kutawasaidia
wajasiriamali kuokoa muda.
Kwa upande wake Hadji Jamadary
Afisa uendeshaji wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF anasema watu
wengi wanajiunga na mfuko huo kutokana na ubora wa mafao yake na faida
inayotolewa kwa mwanachama wa mpango wa hiari.
“PSPF sasa ni kwa watu wote walio
kwenye sekta rasmi na wale ambao hawako kwenye sekta rasmi maana lengo
letu ni kuwafikia watu wengi ndani na nje ya nchi kupitia mpango huu wa
uchangiaji wa hiari (PSS) ambao kiwango cha chini cha uchangiaji ni
sh.10,000.” anasema Bw. Jamadary.
Aidha Mafao katika mpango huo wa
hiari mwanachama atastahili kulipwa michango pamoja na riba
inayokokotolewa kwa mujibu wa viwango vya riba vilivyoko katika soko
kulingana na mfumuko wa bei.
Anasema mafao yaliyopo katika
mpango wa hiari ni ya aina sita (6) kama vile fao la elimu ambalo
litatolewa kwa mwanachama ambaye amechangia kwenye mfuko kwa kipindi
kisichopungua miezi kumi na mbili (12). Nusu ya akiba ya mwanachama
yaani asilimia 50 ya mchango inatumika kulipa fao hili na nusu yake
inayobaki katika akaunti ya mwanachama hutumika kwa ajili ya akiba ya
uzeeni.
Kwa upande wa fao la ujasiriamali
linatolewa kwa mwanachama ambaye amechangia kwenye mfuko kwa kipindi
kisichopungua miaka kumi na mbili (12). Nusu ya akiba ya mwanachama
yaani asilimia 50 ya mchango inatumika kulipa fao hili na nusu yake
inayobaki katika akaunti ya mwanachama hutumika kwa ajili ya akiba ya
uzeeni.
Mpango huo wa hiari Mwanachama
anapata hata fao la uzeeni ambalo hulipwa kwa mwanachama aliyefikisha
miaka 55 au zaidi. Mwanachama analipwa akiba yake ya asilimia mia moja
(100%) pamoja na riba itakayokokotolewa. Mwanachama anapaswa kujaza fomu
ya maombi na kuambatanisha kitambulisho cha uanachama.
Fao la kifo hulipwa kwa wategemezi
wa mwanachama aliyefariki. Malipo yanayolipwa ni ya asilimia mia moja
(100%) ya akiba ya mwanachama na riba inayokokotolewa.
Aidha Wategemezi wanapaswa
kuwasilisha cheti cha kifo, kitambulisho cha uanachama cha marehemu
pamoja na nyaraka za mahakama zinazodhibitisha msimamizi wa mirathi na
wategemezi wa marehemu pamoja na mgao wa mirathi.
Fao la ugonjwa au ulemavu huwa
linatolewa kwa mwanachama ambaye kutokana na sababu za ugonjwa au
ulemavu hataweza tena kumudu kufanya kazi za uzalishaji kwa ajili ya
kujipatia kipato cha kila siku.
Mwanachama analipwa asilimia mia moja (100%) ya akiba yake pamoja na riba inayokokotolewa. Mwanachama anawasilisha barua ya maombi, kitambulisho cha uanachama na uthibitisho wa taarifa ya daktari.
Mwanachama analipwa asilimia mia moja (100%) ya akiba yake pamoja na riba inayokokotolewa. Mwanachama anawasilisha barua ya maombi, kitambulisho cha uanachama na uthibitisho wa taarifa ya daktari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global
Publishers, Eric Shigongo, ambaye ana washawishi wananchi kujiunga na
huduma hiyo aliwaasa wajasiriamali mbalimbali wakiwemo wanasoka,
waendesha bodaboda, wavuvi na wengineo kujiwekea akiba kupitia mpango
huo.
Bi. Rahel Chizoza mwanahabari wa
Clouds Media anasema Uchangiaji kwa kutumia mfumo wa MaxMalipo
unaumuhimu mkubwa katika jamii kwa ujumla kwani unashirikisha sekta
rasmina isiyo rasmi na utakuwa ndio nguzo mojawapo ya kujiongezea kipato
na hata kujiwekea akiba ya uzeeni ikiwa ni pamoja na kuokoa muda wa
mchangiaji kusafiri umbali mrefu.
‘Huduma hii ni nzuri sana ndugu
mwandishi kwani tumekuwa tukiacha shughuli zetu za uzalishaji mali na
kusafiri kwa umbali mrefu ili kujua kiasi cha michango tunayochangia
lakini kwa sasa PSPF wameturahisishia maana hata nikiwa Mafia sina haja
ya kuja Dar es Salaam au kutoka Kijijini kuja mkoani kwa ajili ya kupata
huduma ya kuchangia.Anasema Bakari Mbilambi mwanachama wa mfuko huo.
Mfuko wa pensheni wa PSPF una
uzoefu wa muda mrefu katika sekta ya hifadhi ya jamii tangu Julai 1999
na umekuwa na mafanikio makubwa hadi kuanzisha Mpango wa Uchangiaji wa
Hiari mwezi Februari 2013.Hadi kufikia mwezi Juni 2015.Mpango huu
umesajili zaidi ya wanachama 38456.
Makala haya yameandikwa na
Benjamin Sawe, Afisa Habari, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, email sawebenjamin@gmail.com, simu: 0718028790

0 comments :
Post a Comment