Hatua ya Robo Fainali ya michuano
ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa
kuanza kesho Jumanne kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Mchezo wa kwanza utakua ni kati
ya Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR ya Rwanda
itakayotoshuka dimbani saa 7:45 mchana kucheza na vijana wa Kwesi Appiah
timu ya Al Khartoum kutoka nchini Sudan.
Saa 10:15 kamili jioni, Gor Mahia
mabingwa wara tano wa michuano ya Kagame watashuka dimbani kucheza na
Malakia kutoka Sudan Kusini, viingilio vya michezo hiyo ya jumanne cha
chini kitakua ni elfu tatu (3,000) na kiingilio cha juu kitakua ni elfu
kumi na tano (15,000).
Robo fainali zitaendela siku ya
jumatano, ambapo michezo miwili itachezwa katika uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam huku macho na masikio ya wapenzi wa mpira Afrika Mashariki
yakielekezwa kwa mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
Kabla ya mechi hiyo ya wapinzani
wa soka nchini Tanzania kuchezwa majira ya saa 10 jioni, mchezo wa
kwanza utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy kutoka
nchini Sudan.
Viingilio vya mchezo wa siku ya
jumatano, kiingilio cha chini ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilo
cha juu kitanua ni elfu ishirini (20,000).
Katika hatua hiyo ya robo fainali
endapo timu zitacheza kwa dakika 90 na mchezo kumalizika kwa sare,
hatua itakayofuata ni kumpata mshindi kwa matuta (penati).
CECAFA YAIPA ONYO GOR MAHIA
Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi
za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiandika barua ya onyo klabu ya
Gor Mahia kutoka nchini Kenya kufuatia kuonyesha vitendo vya utovu wa
nidhamu katika michezo yake miwili ya kwanza.
Katika barua hiyo ya CECAFA
kwenda kwa Gor Mahia, imeutaka uongozi huo kuhakikisha kocha wake Frank
Nutal na kikosi kizima kinafuata taratibu za mashindano na kanunu
zilizopo zinazoongoza michuano hiyo.
Kamati ya uendeshaji wa michuano
hiyo (LOC) iliwasilisha malaliko kwa uongozi wa CECAFA juu ya tabia ya
utovu wa nidhamu iliyoonyeshwa na kocha mkuu wa Gor Mahia, na kitendco
cha kuvunja kitasa cha mlango ili kuingia uwanjani.
ZUNGU AZINDUA AIRTEL RISING STAR
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu leo
amezindua michuano ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dare salaam, ambapo
timu kutoka wiliya za Ilala, Temeke na Kinondoni zinashikriki michuano
hiyo.
Akifungua michuano hiyo, Zungu
amewatka vijana kutumia vizuri nafasi hiyo ya michuano ya Airtel Rising
kuonekana, kwani kutawapelekea kupata nafasi ya kucheza katika timu
kubwa na kuweza kuendesha maisha yao kwa kupitia mpira wa miguu.
Michuano ya Airtel Rising Stars
imekua ikifanyika kila mwaka nchini kwa lengo la kusaka na kuibuka
vipaji vya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, ambapo wachezaji
wenye vipaji huchaguliwa na kupelekwa katika vituo vya kufundisha soka
na wengine huchaguliwa katika kikosi cha Taifa cha Vijana (Serengeti
U17)

0 comments :
Post a Comment