Mjini Wanasema ' Ushamba Mzigo', Na Ni Hivi...


Published @nkupamah blog
Shule Duniani Haijawahi Kumsaidia Mwanadamu Kuushusha Hadi Chini' Mzigo Wa Ushamba!'
Ndugu zangu,
Kuna ambao wamekwenda shule kidogo sana, au hawajaingia kabisa darasani, lakini wana akili ya maisha. Na wala si washamba. Na kuna waliokwenda shule wakawa na digrii zaidi ya moja, lakini, ni washamba kweli.

Naam, duniani hapa shule haijawahi kumwondolea mwanadamu ushamba wake. Na ajabu ni kwamba, washamba wengi wako mijini!
Nakumbuka miaka ile ya 80 katikati. Nilikuwa nafuatilia gazetini kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge; Martha Wejja Versus Kitwana Kondo. Issa Shivji alikuwa wakili wa kujitolea wa Martha Wejja kupinga matokeo yaliompa ubunge Kitwana Kondo.
Kwenye cross examination Issa Shivji alianza kumuuliza maswali aliyekuwa DC wa Ilala Captain Mapunda;
Issa shivji: " Jina lako nani?"
DC Mapunda: " Naitwa Captain ( Sikumbuki jina la kwanza) Mapunda"
Issa Shivji: " Na Captain nalo ni jina lako?"
DC Mapunda: " Si vibaya kutaja cheo changu"
Issa Shivji: " Nimekuuliza jina lako nani?"
Naam, mabishano ya jina na cheo cha anaeulizwa kuchanganywa na jina yalichukua dakika kadhaa.
Hakika, ' Ushamba Mzigo, Na Duniani Hapa Shule Haijawahi Kumsaidia Mwanadamu Kuushusha Hadi Chini, Mzigo Wa Ushamba!
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment