Mwanamuziki Peter Okoye wa kundi la P-Square.
HABARI za
vipigo miongoni mwa wanandoa nyota na kuvunjika kwa ndoa zao zimekuwa
zikiongezeka kila kukicha nchini Nigeria, jambo ambalo limemfanya
mwanamuziki
Peter Okoye wa kundi la P-Square kulivalia njuga akitaka
likome. (P.T)
Katika kuonyesha anavyochukia hali hiyo, Okoye ametengeneza T-Shirt inayolaani ‘Vipigo Majumbani kwa Wanandoa’.
Katika tukio moja la namna hiyo hivi majuzi ni pale mtangazaji wa Cool FM OAP Freeze aliposema kwamba mkewe amekuwa akimpiga kila mara na kumsababishia makovu.
Katika tukio moja la namna hiyo hivi majuzi ni pale mtangazaji wa Cool FM OAP Freeze aliposema kwamba mkewe amekuwa akimpiga kila mara na kumsababishia makovu.
Vilevile ndoa ya mwigizaji maarufu wa Nigeria, Emeka Ike iko shakani
baada ya mkewe kudai talaka kutokana na manyanyaso anayofanyiwa na
mumewe huyo.
Pamoja na
picha ambayo amevaa T-Shirt na kuiweka kwenye mtandao wa Instagram,
Okoye aliongeza maneno: “Nyumba ambayo mwanamke hayuko salama si nyumba
ya kuishi.
Wanaume
pia nao hujikuta wakikutana na vipigo kutoka kwa wake zao. Si wanawake
tu ambao huathirika na vipigo, bali wanaume pia huathirika na matusi na
maudhi mbalimbali – lakini huogopa kuomba msaada.”


0 comments :
Post a Comment