Mratibu
wa Burudani wa Club mpya ya 'Maisha Basement' zamani New Club Maisha
pamoja na Maisha Club za Tanzania, Hemed Kavu (katikati), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu
uzinduzi wa Club hiyo utakaofanyika Idd Mosi katika Jengo la LAPF Towers
lililopo mkabala na Makumbusho ya Taifa eneo la Kijitonyama ambapo
mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Kulia ni Meneja Mkuu wa Miasha Club za Tanzania, Allan Ngugi na Kushoto
ni Meneja Uendeshaji wa Maisha Basement, Sam Kaliuki.
Mratibu
wa Burudani wa Club mpya ya 'Maisha Basement' zamani New Club Maisha,
Hemed Kavu (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Wa kwanza kushoto
ni Meneja wa Burudani, pamoja na Geofrey Gilla na wa kwanza
kulia ni Afisa Mahusiano wa Maisha Club pamoja na Maisha Basement, Omary
Sharifu


Afisa Mahusiano wa Maisha Club pamoja na Maisha Basement, Omary Sharifu, akiwaonesha wanahabari ukumbi huo.
Meneja Mkuu wa Maisha Club Tanzania , Allan Ngugi (kulia),
akiwakwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Club
pamoja Maisha Basement, Jean Claud Ciza wakati wa utambulisho wa
uzinduzi club ya Maisha Basement kwa wanahabari.
Mtaalamu wa mitambo katika Clab hiyo, Mr Dong
akifanya vitu vyake.
Ukumbi huo unavyonekana kwa ndani.
Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, anatarajia kuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Club mpya ya 'Maisha Basement'. iliyopo katika Jengo
la LAPF Towers lililopo mkabala na Makumbusho ya Taifa eneo la
Kijitonyama jijini Dar es Salaam
Hafla
ya uzinduzi wa club hiyo zamani ikujulikana kama 'New maisha Club'
utafanyika siku ya Idd Mosi katika ukumbi huo ambapo watu mbalimbali
wamealikwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Mratibu wa
Burudani wa Club hiyo, Hemed Kavu, alisema uzinduzi utafanyika kwa siku
tatu tofauti ambazo ni leo, kesho na kilele ni siku siku hiyo ya Idd
Mosi.
Alisema
club hiyo mpya ambayo ni ya kisasa inauwezo wa kuchukua watu zaidi 700
kwa wakati mmoja na imejengwa katika kiwango cha kimataifa.
"Katika
Siku hizi zote za uzinduzi kutakuwa na burudani mbalimbali...club yetu
ina vifaa vya kisasa na dance floor ya kisasa yenye uwezo wa kurusha
matukio moja kwa moja kama video na mechi na ina maegesho ya magari
hivyo kuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa mali za wateja" alisema.
Alisema
hivi sasa wamekuja tofauti na walivyokuwa maisha club Masaki, kwani
burudani zao zilikuwa zinaanza Jumatano mpaka Jumapili, lakini sasa
zitaanza Jumatatu mpaka Jumatatu huku kiingilio kikiwa ni sh. 10,000 kwa
siku zote.
Akitaja
ratiba zao, alisema siku ya Jumatatu watakuwa na 'Blue Monday nite' kwa
ajili ya wale wanaofanya kaz mwishoni mwa wiki, Jumanne 'Meet and Greet
nite' huu ni usiku wa mashabiki kukutana na mastaa mbalimbali na
Jumatano ni usiku wa Figisu figisu ambapo kutakuwa na burudani zote za
Kiswahili.
"Alhamisi
ni usiku wa ukae ambao tutakuwa tunapata burudani za bendi zetu za hapa
nyumbani, Ijumaa 'Winngle Nite' usiku wa kupata ngoma za kisasa, RNB na
East Africa Music, Jumamosi 'Ibiza Nite' kutakuwa na muziki wa kihindi
na kiarabu, na Jumapili 'Bongo Swagg' ni usiku wa live performance kwa
wanamuziki wetu," alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za
jamii.com)


0 comments :
Post a Comment